Pata taarifa kuu
ULAYA-USALAMA

NSA iliwapeleleza viongozi wa EU, pamoja na Angela Merkel, "kupitia" Denmark

Marekani iliwapeleleza wanasiasa barani Ulaya, pamoja na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, kuanzia mwaka 2012 hadi mwaka 2014 kwa msaada wa idara za ujasusi za Denmark, vyombo vya habari vya Denmark na Ulaya vimeripoti.

Angela Merkel na simu yake ya rununu, wanayeshukiwa kuwa alifanyiwa udukuzi na NSA.
Angela Merkel na simu yake ya rununu, wanayeshukiwa kuwa alifanyiwa udukuzi na NSA. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waandishi wa habari za uchunguzi nchini Denmark pamoja na mashirika ya habari ya Ujerumani ya NDR, WDR na gazeti la Suddeutsche Zeitung waliripoti jana kwamba Marekani iliwadukua wanasiasa wa Ulaya kwa msaada kutoka kwa Denmark.

Patrick Sensburg hashangazwi na hali hiyo, anasema mwandishi wetu huko Berlin, Pascal Thibaut. Mbunge huyo kutoka chama cha Christian Democrat ambaye aliongoza kamati ya uchunguzi ya bunge (Bundestag) kuhusu udukuzi wa Shirika la Usalama la Kitaifa "National Security Agency" (NSA) amebaini kwamba idara za ujasusi hazina marafiki bali ni masilahi tu.

Rais wa sasa alifanyiwa udukuzi

Maafisa wakuu waliohusika na kufichuliwa kwa udukuzi huu, ambao walimbwa na waandishi wa habari za uchunguzi nchini Ujerumani ambavyo vilishiriki katika utafiti huo, televisheni ya serikali ARD na Gazeti la kila siku la Süddeutsche Zeitung, wanasema hawakujua shughuli za shirika hili la NSA. Tayari ilikuwa inajulikana baada ya Edward Snowden kufichuwa kwamba Marekani ilimdukuwa Angela Merkel, hasa kupitia simu yake ya rununu. Sasa ni wazi kwamba mgombea wa chama cha SPD kwenye nafasi ya ukansela mnamo mwaka 2013 Peer Steinbrück alifanyiwa madhila hayo na vile vile Rais wa sasa wa Jamhuri, Frank-Walter Steinmeier.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.