Pata taarifa kuu
COLOMBIA-FARC-AJALI-USALAMA

Colombia yawapoteza wanajeshi wake tisa katika ajali ya helikopta

Jeshi la Colombia limetangaza kwamba, karibu wanajeshi wake tisa wafariki dunia jana Jumanne katika ajali ya helikopta yenye chapa UH-60 Black Hawk ambayo ilikuwa ikiwasafirisha katika operesheni dhidi ya waasi wa zamani wa FARC katika mkoa wa Guaviare.

"Miili tisa imepatikana," Rais wa Colombia Ivan Duque amesema katika hotuba kwenye televisheni.
"Miili tisa imepatikana," Rais wa Colombia Ivan Duque amesema katika hotuba kwenye televisheni. Présidence colombienne
Matangazo ya kibiashara

Askari wengine sita wamejeruhiwa na wawili wamekosekana.

Uchunguzi umeanzishwa na mamlaka nchini humo kubaini chanzo cha ajali hiyo.

"Miili tisa imepatikana," Rais Ivan Duque amesema katika hotuba kwenye televisheni. "Tuko katika wakati mgumu. Tunatambua ushujaa ambao askari wetu na maafisa wa polisi wanaonyesha katika kutuletea amani na kutuliza nyoyo zetu."

Kundi la wapiganaji wa FARC waliofutilia mbali mkataba wa amani uliosainiwa na kati ya viongozi wa kundi hilo na serikali mnamo mwaka 2016 linaendelea kuepo katika eneo hilo ambalo ajali hiyo ilitokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.