Pata taarifa kuu
VENEZUELA-COLOMBIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Coronavirus: Wakimbizi wa Venezuela waliokimbilia Colombia warejea nchini

Mamia ya raia wa Venezuela ambao walitorokea nchini Colombia kwa sababu ya mdororo wa kiuchumi wa nchi yao wameamua kurudi nchini, wakati huu ugonjwa wa Covid-19 ukiendelea kuzua wasiwasi duniani.

Kwenye daraja la Simon-Bolivar, mpaka kati ya Venezuela na Colombia (picha ya kumbukumbu).
Kwenye daraja la Simon-Bolivar, mpaka kati ya Venezuela na Colombia (picha ya kumbukumbu). REUTERS/Carlos Eduardo Ramirez
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi na Jumapili mamia ya raia hao walirejea nchini Venezuela, kufuatia dharura ya kiafya inaohusishwa na janga la Covid-19 (Corona), kulingana na mamlaka ya uhamiaji nchini Colombia.

Jumamosi Aprili 4, watu 600 walipitia kwenye daraja la kimataifa la Simon-Bolivar huko Cucuta (kaskazini mashariki), na wengine 160 walirejea nchini kwa miguu wakitumia barabara kutoka Bogota Aprili 5, kwa mujibu wa shirika la habari la Migracion Colombia. Kundi kubwa zaidi, linaloundwa na wanawake 167 na watoto 35, walisafiri kwenda Cucuta kutoka mji wa karibu wa Bucaramanga kwa msaada wa viongozi.

Kabla ya kuvuka daraja la Simon-Bolivar, wakimbizi hao wa Venezuela walio kuwa walivaa mask walifanyiwa vipimo ili kuona kwamba wanaweza kuwa wameambukizwa virusi vya Corona.

Licha ya Colombia kufunga mipaka yake kutokana na janga la Covid-19, raia hao walitakiwa kutumia njia zilizotengwa na serikali ili kuweza kufika katika maeneo yaliyo tengwa kwa ajili ya kuwapôkea ria wake wanaorejea kutoka ukimbizini wakati huu ugonjwa wa Covid-19 ukiendelea kuzua wasuwasi kubwa duniani.

Takribani wahamiaji milioni 4.9 kutoka Venezuela kote ulimwenguni wanahitaji msaada wa kimataifa kutokana na athari za kiuchumi kufuatia janga hilo, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa. Nchini Colombia, zaidi ya visa 1,400 vya maambukizi na vifo 35 vinavyohusiana na ugonjwa wa Covid-19vimeripotiwa tangu Machi 6.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.