Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Trump Junior: Baba hakufahamu lolote kuhusu mkutano wangu

Mtoto wa rais wa Mareani Donald Trump, Trump Junior, siku ya Jumanne Julai 11, alichapisha kwenye Twitter, mfululizo wa barua pepe zikionyesha kuwa alikaribisha ombi la kukutana na wakili, ambaye alikuwa na uhusiano na Urusi, ambaye alikuwa na ujumbe potovu kumhusu Hillary Clinton wakati wa kampeni za uchaguzi.

Baadhi ya barua pepe mtoto wa kwanza wa Donald Trump alizochapishwa siku ya Jumanne Julai 11 kwenye Twitter.
Baadhi ya barua pepe mtoto wa kwanza wa Donald Trump alizochapishwa siku ya Jumanne Julai 11 kwenye Twitter. DonaldJTrumpJR/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Pendekezo hilo lilipokelewa kwa furaha na mwanae Donald Trump. Kesi hii imezua mvutano katika bunge la Congress, wakati ambapo uchunguzi kuhusu kampeni kati ya Trump na Urusi unaendelea

Gazeti la New York Times ambalo lilifichua mkutano huo wa Donald Junior na wakili wa Urusi, lilikuwa katika hatua ya kuthibitisha ukweli kuhusu uchunguzi wake.

Donald Trump Jr, mkwe wake Jared Kushner na mwenyekiti wa kampeni Paul Manafort, walikutana na wakili wa Urusi Natalia Veselnitskaya, katika jumba la Trump Tower mjini New York mwezi Juni mwaka 2016.

Wakati huo huo rais wa Marekani Donald Trump amesem akuwa hakufahamu lolote kuhusu mkurano wa Trump Junior na wakili wa Urusi.

Donald Trump Junior alikiambia kituoa cha habari cha Fox News kuwa mkutano huo haukuhusu chochote.

Hata hivyo Trump Junior, amesema kuwa hakumfahamisha babake kuhusu mkutano na wakili wa Urusi ambaye alisema kuwa angesaidia katika kampeni yake ya uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.