Pata taarifa kuu
MAREKANI-URUSI-USHIRIKIANO

Trump :Putin hajaingilia uchaguzi wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa alipokuatana uso kwa uso na rais wa Urusi Vladimiri Putin, alikana kuwa hajaingilia uchaguzi wa Mareknai au kuvuruga uchaguzi huo, kama wanavyomshtumu.

Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017.
Rais wa Marekani Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, mjini Hamburg, Julai 7, 2017. REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Aliandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa Putin alikana kabisa kuvuruga uchaguzi wa Marekani wakati walikutana uso kwa uso kwenye mkutano wa G20 siku ya Ijumaa.

Madai haya ya rais wa Marekani yanatofautiana na yale ya maafisa wake wa vyeo vya juu katika jeshi na polisi

Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley, amebaini kwamba Marekani haiwezi kuiamini Urusi.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson, alisema kuwa hatua ya Urusi kuvuruga uchaguzi wa mwaka 2016 imesalia kikwazo kikubwa kwenye uhusiano wake na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.