Pata taarifa kuu
BRAZILI-SIASA-UCHUMI

Brazil: kamati maalum yamtaka Dilma Rousseff kuachia ngazi

Pigo jipya kwa Rais wa Brazil Dilma Rousseff. Kamati Maalum inayohusika na kutoa maoni yake juu ya utaratibu wa kujiuzulu kwa rais wa Brazil imetangaza katika neema ya kujiuzulu kwa rais huyo.

Wabunge wa kamati maalum ya bunge wakati wa mjadala Jumatatu hii Aprili 11, Brasilia.
Wabunge wa kamati maalum ya bunge wakati wa mjadala Jumatatu hii Aprili 11, Brasilia. REUTERS/Ueslei Marcelino
Matangazo ya kibiashara

Kamati hii imepitisha ripoti inayopendekeza muendelezo wa mchakato wa utaratibu wa kumng'oa Dilma Rousseff.

Mjadala mkali ulidumu kwa masaa kadhaa, huku ukikatishwa mara nyingi na wafuasi wanauunga mkono au wanaopinga kuijuzulu kwa Rais Dilma Rousseff. Wafuasi hao, kila upande umekua ukiimba nyimbo na kushikilia mabango.

Kura ya Wabunge wa tume maalum itaruhusu mchakato wa kujiuzulu kuweza kujadiliwa na kupigiwa kura katika kikao cha hadhara cha Wabunge wote. Kura muhimu inaweza kufanyika Jumapili wiki hii au Jumatatu ijayo.

Kwa hiyo, mashaka yanaendelea nchini Brazil. Kura hii katika neema ya mashtaka dhidi ya Dilma Rousseff inakuja kuongeza shinikizo kwa rais na kuzidisha tena mgogoro wa kisiasa unaoikabili nchi hii kwa miezi kadhaa. Rais Dilma Rousseff anashutumiwa kutumia akaunti za umma ili kusaidia uchaguzi wake mwaka 2014.

Kama Baraza la Bunge limepiga kura kwa ajili ya kutimuliwa kwa Dilma Rousseff, hatua inayofuata ni ya Baraza la Seneti kuchukua uamuzi.

Rais wa Brazil anaweza kuondolewa madarakani kwa muda, hadi mwisho wa uchunguzi. Makamu wake wa Rais, Michel Temer, tayari ameanza kujiandaa kushikilia nafasi hiyo. Yeye ndiye anapaswa kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi iwapo Dilma Rousseff atatimuliwa mamlakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.