Pata taarifa kuu
BRAZILI-UCHUMI-RUSHWA-SIASA

Brazil: chama cha PMDB chajiondoa katika muungano wa Dilma Rousseff

Chama kikuu cha mrengo wa kati nchini Brazil cha PMDB, Jumanne hii kimepigia kura ya kujiondoa katika muungano wa Rais wa mrengo wa kushoto Dilma Rousseff, anaye kabiliwa na tishio la kujiuzulu.

Wabunge wa chama cha PMDB wakipongeza uamuzi wa chama chao wa kujiondoa katika muungano wa Rais Dilma Rousseff, Brasilia tarehe 29 Machi.
Wabunge wa chama cha PMDB wakipongeza uamuzi wa chama chao wa kujiondoa katika muungano wa Rais Dilma Rousseff, Brasilia tarehe 29 Machi. REUTERS/Adriano Machado
Matangazo ya kibiashara

Uongozi wa chamacha PMDB, mshirika muhimu wa chama cha Wafanyakazi cha PT cha mrengo wa kushoto (kilio madarakani), ulikutana jumanne hii mchana katika mji mkuu wa Brazil, Brasilia ili kukamili kujiondoa huko katika muungano. Rais wa Brazil amefuta safari ya Marekani ambako angelihudhuria mkutano wa kilele kuhusu usalama wa nyuklia.

Uongozi wa chama cha PMDB kilichukua dakika chache ili kutoa msimamo wake wa kupiga kura ya kujiondoa katika muungano wa Rais Dilma Rousseff. Baada ya miezi kadhaa ya kusita, chama kikuu cha mrengo wa kati,mshirika muhimu wa Rais wa Brazil hatimaye kimeamua kupiga kura ya kujiondoa katika muungano na chama tawala.

Tukio la kwanza la historia

Chama cha PMDB kimeamua kuondoa mawaziri wake kutoka serikalini. Uongozi wa chama cha PT katika ngazi ya taifa, chama cha Makamu wa Rais Michel Temer, ambaye atamrithi Rousseff kama atatimuliwa madarakani na Bunge, kimeamua "kujiondoa haraka katika serikali", huku akitolea wito mawaziri wake kujiuzulu.

"Kuanzia leo, katika mkutano huu wa kihistoria wa chama cha PMDB, PMDB inajiondoa katika serikali ya Rais Dilma Rousseff na mtu yeyote katika nchi hii haruhusiwi kushikilia nafasi yoyote kwa jina la chama cha PMDB" , amesema naibu kiongozi wa chama, Romero Juca. Tukio la kwanza tangu mwisho wa udikteta na kurudi kwa demokrasia mwaka 1985, uamuzi ulioelezwa wa kihistoria na Seneta wa chama cha PMDB Seneta anayehusika na zoezi la kupiga kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.