Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA-RUSHWA

Pigo jipya kwa Rais wa Brazil Dilma Rousseff

Utaratibu wa kumng'oa Rais wa Brazil Dilma Rousseff umeingia hatua mpya. Kabla ya kura ya Wabunge, kamati maalum ya Bunge inayohusika na kutathmini utaratibu pamoja na mwandishi wake wametoa msimamo wao, Jumatano, Aprili 6, katika neema ya kumuangusha Rais Rousseff. Pigo jipya kwa chama tawala.

Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Aprili 5, 2016 katika mji mkuu wa Brasilia.
Rais wa Brazil Dilma Rousseff, Aprili 5, 2016 katika mji mkuu wa Brasilia. REUTERS/Adriano Machado
Matangazo ya kibiashara

Dilma Rousseff anaonekana kuwa haungwi tena mkono na baadhi ya taasisi za uongozi wa nchi. Mbele ya tume maalum ya bunge inayohusika na kujadili kukubaliwa kwa mashtaka dhidi ya Rais, Jovair Arantes, amesema kuna ulazima wa kuendelea kwa utaratibu wa kumng'atua madarakani Rais Dilma Rousseff.

Kikao kilichoendeshwa na mwandishi wa kamati hiyo ya Bunge, kilikua na mvutohuku akionekana kuunga mkono kwa neema ya kujiuzulu kwa Rais Rousseff, jambo ambalo huenda likasababisha nchi ya Brazili kukumbwa na hali ya sintofahamu. "Kazi yangu haikuwa rahisi. Baadhi watanambia kuwa mimi ni shujaa. Wengine watasema nimehusika na mapinduzi. Nina uhakika kuwa nitaamsha hisia ya kila raia wa Brazil, mbaya zaidi kama nzuri, " Jovair Arantes amesema.

Makamu wa rais pia atishiwa

Wabunge 65 wa kamati maalum wataamua mapema wiki ijayo kama wafuata msimamo wa mwandishi wa kamati hiyo kwa kuwataka Wabunge wote wapige kura ya kung'atuliwa madarakani Rais Dilma Roussef.

Mashaka yanaendelea kukua. Makamu wa Rais Michel Temer pia analengwa na ombi la kujiuzulua, kwa jitihada za Jaji wa Mahakama Kuu. Na inasemekana kuwa huenda akachukua hatamu ya uongozi wa nchi, kama Dilma Rousseff atakua ameng'atuliwa madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.