Pata taarifa kuu
BRAZIL-SIASA-RUSHWA

Hatma ya Dilma Rousseff mikononi mwa Wabunge

Wiki muhimu inaanza kwa Rais wa Brazil Dilma Rousseff pamoja na kupiga kura leo Jumatatu kwa Kamati ya Bunge kuhusu kutimuliwa kwake kabla ya wabunge kupiga kura katika kikao chao cha pamoja kuanzia siku ya Ijumaa wiki hii.

Wabunge wa upinzani wakishikilia mabango na vitu ambavyo wanavifananisha na Rais wa zamani Inacio Lula da Lula wakati wa kikao cha Kamati Maalum Aprili 6, 2016 katika mji wa Brasilia.
Wabunge wa upinzani wakishikilia mabango na vitu ambavyo wanavifananisha na Rais wa zamani Inacio Lula da Lula wakati wa kikao cha Kamati Maalum Aprili 6, 2016 katika mji wa Brasilia. EVARISTO SA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kamati maalum ya wabunge 65 watapitisha kwa idadi kubwa rahisi, kuanzia saa 11:00 jioni (sawa na saa 3:00 usiku saa za kimataifa), ripoti isio ya kisheria kwa muendelezo wa mchakato wa kuondolewa kwa kiongozi kutoka chama cha mrengo wa kushoto mbele ya Baraza la Seneti ambalo litakua na uamuzi wa mwisho.

Rousseff, mwenye umri wa miaka 68, mpiganaji wa zamani wa maguguni chini ya utawala wa udikteta wa kijeshi, anatuhumiwa na upinzani kutumia fedha za umma mwaka 2014, mwaka ambapo alichaguliwa, na katika mwaka 2015, ili kupuuzia ukubwa wa mapungufu ya umma unaoikabili chini hii ya Amerika ya Kusini hasa katika uchumi wake.

Rais wa Brazil anakanusha tuhuma hizo na kujitetea kuwa hajafanya "uhalifu wowote wa kimadaraka" unaohalalisha kujiuzulu kwake na amelaani jaribio la "mapinduzi ya kitaasisi."

Katibu wa Kamati Maalum, Mbunge kutoka mrengo wa kulia, Jovair Arantes, aliunga mkono Jumatano wiki iliyopita mbele ya Baraza la Seneti tuhuma zinazomkabili Rais Dilma Rousseff.

Ripoti ya tume maalum itawasilishwa kuanzia Ijumaa mbele ya Wabunge ambapo huenda ikapigiwa kura Jumapili wiki hii au Jumatatu ya wiki ijayo.

Theluthi mbili ya kura za Wabunge (342 kwa jumla ya 513) zinahitajika ili utaratibu huo ufuate mkondo wake, vinginevyo utaratibu huo utafutiliwa mbali kabisa.

Makamu wa Rais Michel Temer, mwenye umri wa miaka 75, ndiye atachukua hatamu ya uongozi wa nchi hadi mwisho wa muhula wake iwapo utaratibu huo utapitishwa na idadi hiyo ya Wabunge pamoja na Baraza la Seneti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.