Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

DRC: Mwanajeshi mmoja auawa Djugu katika vita kati ya FARDC-MONUSCO dhidi ya CODECO

Mwanajeshi mmpja aliuawa kwa kupigwa risasi siku ya Alhamisi, Aprili 11, na wanamgambo wa CODECO ambao walishambulia ngome ya jeshi, iliyoko karibu na Drodro, katika eneo la Djugu katika mkoa wa Ituri, Kaskazini Mashariki mwa DRC.

Wanajeshi wa DRC, FARDC, Wakipiga kambi katika moja ya maeneo ya Djugu, Kaskazini Mashariki mwa DRC.
Wanajeshi wa DRC, FARDC, Wakipiga kambi katika moja ya maeneo ya Djugu, Kaskazini Mashariki mwa DRC. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kulingana Radio OKAPI inayorusha matangazo yake nchini DRC, ikinukuu vyanzo vya usalama, vikosi vyaserikali vilijibu na kuwarudisha nyuma watu hawa wenye silaha ambao walikuwa wakijaribu kusonga mbele kuelekea hospitali na eneo la watu waliohama makazi yao kutoka Drodro.

Baada ya kufahamishwa, walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, kutoka kituo cha Drodro walitumwa kusaidia FARDC.

Majibizano haya ya risasi yalidumu karibu saa tatu kabla ya muungano wa FARDC-MONUSCO kuwarudisha nyuma wanamgambo wa CODECO.

Washambuliaji hawa walirudi nyuma kuelekea kilima cha Tata.

Utulivu wa hali ya juu umeonekana tangu siku ya Ijumaa asubuhi katika eneo hili, ambapo FARDC na askari wa MONUSCO wameimarisha doria kwa ajili ya ulinzi wa raia.

Harakati kubwa ya wanamgambo wa CODECO ilikuwa imezingatiwa kwa takriban wiki moja katika baadhi ya maeneo katika eneo la Djugu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.