Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Katika Goma iliyozingirwa, wanajeshi na wanamgambo washambulia raia

Kila asubuhi huko Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, raia huhesabu idadi ya vifo, waathiriwa wa uporaji na unyanyasaji wa kijinsia wakati wa usiku. Wakiwa wamekasirishwa, wakaazi hao wanashutumu askari wa kikosi cha walinzi wa Jamhuri na wanamgambo wanaoshika doria katika jiji hilo lililozingirwa na waasi wa M23

Goma inasemekana kuwa na zaidi ya wakazi milioni moja na karibu watu milioni moja waliokimbia makazi yao kutokana na vita, wamejazana katika kambi zisizo safi nje kidogo ya jiji hilo, ambazo zimekuwa uwanja wa vita.
Goma inasemekana kuwa na zaidi ya wakazi milioni moja na karibu watu milioni moja waliokimbia makazi yao kutokana na vita, wamejazana katika kambi zisizo safi nje kidogo ya jiji hilo, ambazo zimekuwa uwanja wa vita. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika video, kijana anajiviringisha chini, akivuja damu hadi kufa. Karibu na eneo la tukio, mwingine amelala kwenye dimbwi la damu. Vilio vya wanawake vinasikika usiku kucha huko Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kama kila asubuhi, wakaazi wa jiji hilo huamka kila mmoja akiuliza mwenziye idadi ya watu waliouawa, kubakwa au kuibiwa usiku.

"Nani aliua? Nani aliuawa? Ilikuwa katika kitongoji gani?" , wanajiuliza wakaazi wa mji wa Goma katika makundi ya mazungumzo ya mtandaoni, ambapo video za watu waliouawa huzunguka. Mazungumzo hayo huambatanishwa na maneno  "Ee Mungu wangu!", kama kilio cha kutokuwa na uwezo wa kukabiliana dhidi ya kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, ambao leo umezungukwa na waasi wa M23 na vitengo vya jeshi la Rwanda, kulingana an vyanzo kadhaa.

Goma inasemekana kuwa na zaidi ya wakazi milioni moja na karibu watu milioni moja waliokimbia makazi yao kutokana na vita, wamejazana katika kambi zisizo safi nje kidogo ya jiji hilo, ambazo zimekuwa uwanja wa vita. "Watatu wamekufa!", afisa wa polisi kutoka wilaya ya Majengo ameliambia shirika la habari la AFP, ambapo vijana wanaoonyeshwa katika video waliuawa siku ya Jumanne jioni, walipokuwa wakitazama mechi ya Real Madrid dhidi ya Manchester City kwenye duka.

Papo hapo, kila mtu yuko wazi: "Ni askari kutoka kikosi cha Walinzi wa Jamhuri ndiye aliyewaua." "Alitaka kuwanyang'anya simu," anasema Christian Kalamu, kiongozi wa shirika la kiraia katika eneo hilo. "Inadaiwa walipinga kunyang'anywa simu zao na akawafyatulia risasi," ameongeza.

Askari wa kikosi cha walinzi wa Jamhuri ni sehemu ya kinadharia ya wasomi wa jeshi la Kongo, ambalo linatumwa mashariki kujaribu kuwaondoa waasi ambao, kwa msaada wa Rwanda, wameteka maeneo makubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

"Wanatupiga risasi"

Wakiongozwa, FARDC (Vikosi vya Wanajeshi vya DRC) walitoa wito kwa makundi makuu yenye silaha katika eneo hilo, ambayo walikuwa wakishirikiana nayo miezi michache iliyopita katika vita dhidi ya M23. Wakifahamika kwa jina la "wazalendo", kwa wazo la kufuta uhalifu wa kivita wa baadhi ya watu, wanamgambo hawa hupokea silaha na risasi kutoka kwa mamlaka, ambayo pia huratibu operesheni, kulingana na ripoti mbalimbali, kutoka Umoja wa Mataifa hasa.

Mwishoni mwa mwezi wa Machi, Rais wa DRC Félix Tshisekedi aliwaambia waandishi wa habari kuhusu wazalendo: "Hao ni raia wa kawaida kama wewe na mimi, waliojipanga."

Wakiwa wamejificha katika mji wa Goma, maelfu ya watu hao wenye silaha wanajikuta wakizungukazunguka jiji hilo na viunga vyake. "Wakati wa usiku, hutupiga risasi katika makao yetu," analalamika mwanamke aliyehama makazi yake kwa sharti la kutotajwa jina. Miongoni mwa washambuliaji, "kuna askari wa serikali, lakini pia polisi, wazalendo na baadhi ya vijana kutoka mjini", ameongeza, "wote wamechanganyika".

"Baadhi hutembelea kayika vituo vya unywaji pombe mara kwa mara katika kambi, na katika hali ya ulevi, wanaanza kufyatua risasi kwa sababu ya kutoelewana kati yao au kati yao na raia," anaeleza Safari Mbalibukira, chifu wa wilaya ya Mugunga, magharibi mwa jiji. "Ikiwa wanataka simu, redio, pesa au kitu kingine chochote, askari na wazalendo hawavumilii upinzani wowote," anaeleza mmoja wa vijana waliolazimika kutoroka makazi yao.

Wakiwa na hasira, mnamo Machi 5, watu waliokimbia makazi yao walimuua kwa mawe na kumchoma moto mwanamgambo ambaye walimtuhumu kwa kumbaka mwanamke mmoja, kisha kumuua mtu aliyelazimika kuyahama makazi yake ambaye alikataa kuibiwa. "Tumetoka kwenye wizi rahisi hadi kwa vitendo vya uhalifu wa kweli, ikiwa ni pamoja na mauaji na ubakaji," anasema Onesphore Sematumba, mkazi wa Goma na mtafiti katika shirika International Crisis Group, kituo cha kimataifa cha utafiti chenye makao yake nchini Ubelgiji. "Wazalendo wanachochea utovu wa usalama kwa kupora bidhaa chini ya ulinzi kutokana na kujitolea kwao 'kizalendo'," anaongeza mtafiti huyo.

Siku ya Jumatano, mchana kweupe na mita mia chache kutoka ofisi ya gavana, kundi la watu waliokuwa na silaha lilifyatulia risasi dhii ya gari ndogo nyeusi aina ya 4x4 na kuwaua watu watatu waliokuwa ndani yake. Mwanamke aliyekuwa akipita kwa pikipiki karibu na eneo la tukio pia aliuawa. Siku iliyofuata, Meya wa Goma alionyesha askari watatu na wazalendo wawili kwa waandishi wa habari kuwa ndio wahusika wa tukio hilo. Chini kulikuwa na silaha ambazo zilitumika katika uhalifu huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.