Pata taarifa kuu

Viongozi wawili wa ADF wameuwa katika oparesheni mashariki ya DRC

Uongozi wa jeshi la pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na Uganda linalopambana na kundi la ADF, unasema umefanikiwa kuwauwa viongozi wakuu wawili wa kundi hilo linalofungamana na islamic state.

Mamlaka inasema viongozi wa ADF wameuwa katika oparesheni dhidi ya kundi hilo.
Mamlaka inasema viongozi wa ADF wameuwa katika oparesheni dhidi ya kundi hilo. © ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wameripoti kuuawa mapema mapema wiki hii wametajwa kuwa Doctor Musa, na Commander Baghdad

Wilayani Beni katika eneo la Eringeti, katika mpaka wa majimbo ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Katika operesheni ya pamoja, waliyoipa jina Shujaa, wanajeshi wa nchi hizo mbili wanasema walifanikiwa baada ya kufanya msako dhidi ya waasi hao wenye asili ya Uganda kwenye bonde la Mwalika na Rwenzori.

Serikali ya DRC na washirka wake wamekuwa wakipamabana na makundi ya waasi mashairki ya taifa hilo.
Serikali ya DRC na washirka wake wamekuwa wakipamabana na makundi ya waasi mashairki ya taifa hilo. © Coralie Pierret / RFI

Hata hivyo, viongozi hao wawili hawapo kwenye orodha iliyotolewa na watalaam wa Umoja wa Mataifa mwaka 2021 kuwa Makamanda wa kundi hilo.

Mpaka sasa ni vigumu kufahamu idadi ya viongozi wa ADF huku Musa Baluku na Lumisa Mohammed wanaoaminiwa kuwa viongozi wakuu wakiendelea kusakwa tangu mwaka 2019.

Soma piaWatano wauawa katika shambulizi la ADF mashariki mwa DRC

Tangu mwishoni mwa mwaka 2021 nchi hizo mbili ziliunganisha vikosi vyake na kuanza operesheni shujaa dhidi ya waasi hao wanaoendelea kusababisha mauaji ya raia.

Hillary Ingati, RFI- Nairobi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.