Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Wanakijiji 7 wauawa katika Mbuga ya wanyama ya Virunga nchini DRC

Wanakijiji saba wameuawa katika Hifadhi ya Virunga ambako walikuwa wameenda kutengeneza mkaa, katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linalokumbwa na mashambulio ya waasi wa M23, kulingana na vyanzo vya ndani siku ya Ijumaa.

Kulingana na wakaazi hao, M23 ("Movement ya Machi 23") inakataza wakazi wa maeneo inayodhibiti kwenda katika Hifadhi ya Virunga kwa misingi kwamba wanamgambo, ambao wanaweza kuchanganyikiwa nao, wana ngome zao katika hifadhi hiyo.
Kulingana na wakaazi hao, M23 ("Movement ya Machi 23") inakataza wakazi wa maeneo inayodhibiti kwenda katika Hifadhi ya Virunga kwa misingi kwamba wanamgambo, ambao wanaweza kuchanganyikiwa nao, wana ngome zao katika hifadhi hiyo. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Waathiriwa, wote wanaume, waatoka katika kijiji cha Karambi, katika eneo la Rushuru, yapata kilomita thelathini kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. "Tuligundua kwamba walikuwa wamefungwa kamba na kuuawa," mkazi mmoja ameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kutoka Goma.

"Waliuawa kwa mapanga siku ya Jumatano, miili yao ilipatikana leo (Ijumaa)," afisa wa eneo hilo amesema. "Wanatoka eneo letu, kulikuwa na Eric, Claude, Toto, na wengine," ameongeza. Walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30. Kulingana na afisa huyu, kwa kukosa njia nyingine za kujikimu, wanaume hao walikuwa wakienda mbugani kutengeneza mkaa unaoitwa “makakala” ambao walikuwa wakiuuza huko Goma.

Wahusika wa mauaji haya hawajatambuliwa rasmi, lakini wakaazi wanashutumu M23, kundi la waasi ambalo, likisaidiwa na vitengo vya jeshi la Rwanda, limeteka sehemu kubwa za mkoa huo kwa miaka miwili, haswa katika eneo la Rutshuru. Kulingana na wakaazi hao, M23 ("Movement ya Machi 23") inakataza wakazi wa maeneo inayodhibiti kwenda katika Hifadhi ya Virunga kwa misingi kwamba wanamgambo, ambao wanaweza kuchanganyikiwa nao, wana ngome zao katika hifadhi hiyo.

Ili kuisaidia kupambana na waasi, jeshi la DRC, FARDC, lilitoa wito kwa makundi yenye silaha yanayojulikana kwa jina la "wazalendo". Hifadhi ya Virunga, hifadhi kongwe zaidi ya asili barani Afrika, iliyoundwa mnamo mwaka 1925, inasifika kwa wanyamapori wake, haswa sokwe wa milimani, na mandhari yake ya ajabu. Pia ni kiini cha migogoro ambayo imekuwa ikisambaratisha mashariki mwa Kongo kwa miaka 30.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.