Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

DRC: Mkuu wa chama cha rais anamshutumu Joseph Kabila kwa kuunga mkono M23

Mkuu wa chama cha rais Augustin Kabuya alimshutumu siku ya Jumamosi Machi 30,rais wa zamani wa Kongo Joseph Kabila kabange kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu Kaskazini baada ya baadhi ya viongozi vijana wa chama cha Kabila kujiunga na waasi katika mkoa wa Kivu Kaskazini, ambao wakiongozwa hasa na aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Corneille Nangaa. Chama cha Kabila kimejitenga na kundi hili jipya la waasi.

Augustin Kabuya, mkuu wa chama cha rais na afisa anayehusika na upashaji habari katika Bunge la taifa la DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa.
Augustin Kabuya, mkuu wa chama cha rais na afisa anayehusika na upashaji habari katika Bunge la taifa la DRC, wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Kinshasa. © Pascal Mulegwa/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa

Mbele ya wanaharakati zaidi ya elfu moja kutoka chama chake, Augustin Kabuya hakusita kuishutumu kambi ya rais wa zamani kuwa nyuma ya waasi wa M23. Katibu mkuu wa UDPS, chama cha rais, hakusita kumshambulia kambi ya rais wa zamani Joesph Kabila. Alienda mbali na kudai kuwa rais wa zamani Kabila hivi majuzi aliikimbia nchi bila kutoa taarifa kwa idara ya uhamiaji. “Haishi hapa tena. Kumbukeni hili mioyoni mwenu, hali hii tunayopitia, siku zote ni Kabila ambaye ndiye chanzo wa hali hii,” alitangaza Augustin Kabuya hasa kabla ya kueleza kuwa rais huyo wa zamani alimwomba mmoja wa viongozi wa Afrika kumuunga mkono kiongozi wa waasi Corneille Nangaa "kwa njia zote za kifedha na vifaa".

Madai haya yalikasirisha kambi ya Kabila. Barbara Nzimbi, mshauri wa mawasiliano kwa rais wa zamani wa DRC, anasema madai haya ni "mazito, hayawajibiki, hayana uhusiano na ni ya kiwendazimu". Chama cha Tshisekedi kinalegalega katika "kuvurugika" na shutuma hizi zinathibitisha tu kushindwa kwake katika uongozi wa nchi, ameongeza.

Washirika kadhaa wa karibu wa rais huyo wa zamani wamesema wawasilisha malalamiko yao mbele ya taasisi husika kwa kukashifiwa hata kama kwa sasa hakuna kilichoamuliwa, anabaini mshirika wa karibu wa Joseph Kabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.