Pata taarifa kuu

DRC: Kiongozi wa M23 ataka kufanya mazungumzo na Kinshasa, Tshisekedi akataa katakata

Sultani Makenga, kiongozi wa waasi wa M23, alivunja ukimya wake Alhamisi Julai 6. Katika video, alizungumza kwa mara ya kwanza tangu kuibuka tena kwa kundi hili la silaha mnamo 2022 na akahakikisha kwamba anaendelea kudai mazungumzo na Kinshasa. Siku hiyo hiyo, Felix Tshisekedi alimpokea mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ambaye alizungumzia mazungumzo kama suluhu ya mzozo wa mashariki mwa DRC. Lakini rais wa Kongo alifutilia mbali hoja hizo: kujadili, ndiyo, lakini si na M23.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi (kulia) alimkaribisha mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, mjini Kinshasa Julai 6, 2023. Katika hafla hii, alisisitiza msimamo wake thabiti dhidi ya M23, ambayo inatafuta mazungumzo na mamlaka.
Rais wa DRC Félix Tshisekedi (kulia) alimkaribisha mwenzake wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, mjini Kinshasa Julai 6, 2023. Katika hafla hii, alisisitiza msimamo wake thabiti dhidi ya M23, ambayo inatafuta mazungumzo na mamlaka. REUTERS - JUSTIN MAKANGARA
Matangazo ya kibiashara

Rwanda "inaishi kutokana na mashambulizi yake ya mara kwa mara dhidi ya DRC", alisema Félix Tshisekedi. “Kukosekana kwa utulivu huku kuna manufaa ya kiuchumi kwa Rwanda, ambayo hata hivyo inakanusha kuhusika katika mzozo huo. Hii ndiyo sababu, ni vigumu sana kujadiliana na Rwanda”, aaliongeza.

Rais wa Kongo anaongeza kuwa zaidi ya hayo, Kigali "inaikejeli" DRC kwa kutuma "kundi dogo la watu binafsi" ambao aliwataja kama "vibaraka" na "wasaidizi" wa jeshi la Rwanda ili kujadiliana na serikali halali na inayotambuliwa. Hoja nyingine iliyotolewa: hakuna swali kwa Kinshasa kurejea katika mapungufu ya siku za nyuma, yaani kufanya mazungumzo na makundi yenye silaha ambayo, muda fulani baadaye, yanachukua tena silaha.

Katika mahojianona mwandishi wa habari wa kujitegemea, kiongozi wa kijeshi wa kundi la waasi la M23 alizungumza kutoka Jomba, huko Rutshuru, eneo lililo karibu na Bunagana, eneo lililo chini ya udhibiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Alibaini kuwa M23 "imefanya kilio chini ya uwezo wake". Inamaanisha: kujiondoa kutoka kwa sehemu ya maeneo yanayokaliwa. Kwa upande wake, kwa hiyo anadai mazungumzo ya moja kwa moja na Kinshasa. Ombi lililotolewa na kundi hili tangu kuanza kwa mashambulizi.

Bila mazungumzo, Sultani Makenga pia anahakikisha kwamba kundi lake halijisikii "kwa namna yoyote" na mchakato wa kuwakusanya pamoja wapiganaji wake na kuwapokonya silaha, hoja iliopitishwa katika mkutano wa mwisho wa wakuu wa EAC, Mei 31.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.