Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

DRC: Ufaransa yalaani 'msaada wa kijeshi wa Rwanda' kwa M23

Ufaransa ilitoa wito siku ya Jumanne kukomesha "uungaji mkono wa kijeshi" wa Rwanda kwa waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), na kulaani unyanyasaji unaofanywa na makundi mengi yanayohatarisha usalama wa eneo hilo.

Waasi wa M23 huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022.
Waasi wa M23 huko Kibumba, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Desemba 23, 2022. AFP - GLODY MURHABAZI
Matangazo ya kibiashara

"Ufaransa inasikitishwa na taarifa zinazothibitisha M23 kuendelea kushikilia baadhi ya maeneo ya mashariki mwa DRC, kuendelea kuungwa mkono kijeshi na Rwanda kwa kundi hili lenye silaha na uwepo wa wanajeshi wa Rwanda kwenye ardhi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tunaomba uungwaji huu mkono wa Rwanda usitishwe mara moja," kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya nje ya Ufaransa.

Waasi wengi kutoka jamii ya Watutsi, M23, wanaotuhumiwa na Umoja wa Mataifa kwa uhalifu mwingi mashariki mwa DRC, walichukua tena silaha mwishoni mwa mwaka 2021 baada ya miaka kumi na kuteka maeneo makubwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, unaopakana na Rwanda na Uganda.

"Ahadi zilizotolewa na wadau mbalimbali wa kikanda lazima sasa zitekelezwe ili kuharakisha zoezi la kuondoka kwa M23 kwenye maeneo wanayodhibiti, kuweka kundi kambini na kuhimiza makundi yote yenye silaha kushiriki katika mchakato wa kitaifa wa kuwapokonya silaha wapiganaji wao na kuwarejesha katika maisha ya kiraia." imeongeza Quai d'Orsay, ambayo imetangaza uwezekano wa "vikwazo dhidi ya wale wanaozuia amani".

Wakati wa safari yake nchini DRC mwezi Machi, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alitoa onyo mjini Kigali, bila hata hivyo kulaani waziwazi Rwanda.

Katika taarifa yake, Quai d'Orsay pia inalaani "unyanyasaji mwingi unaofanywa na makundi yenye silaha yaliyotajwa katika ripoti ya hivi punde ya kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa". Mbali na M23, makundi mengine kama vile Allied Democratic Forces (ADF), Mai Mai au Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR) vinatishia eneo hilo.

Ukiukaji huu "hauwezi kuachwa bila kuadhibiwa", inasisitiza Quai d'Orsay, na kutaka "msaada unaotolewa na wanajeshi wa DRC, FARDC, kwa baadhi ya makundi yenye silaha kama vile FDLR" pia ukomeshwe.

Katika ripoti iliyotolewa Jumatatu, wataalam wa Umoja wa Mataifa walielezea wasiwasi wao juu ya "kukithiri kwa ghasia" na "kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu" mashariki mwa DRC. Pia walibaini kuwa waasi wa ADF walipokea msaada wa kifedha kutoka kwa kundi la Islamic State (IS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.