Pata taarifa kuu

HRW yashutumu M23 kwa kufanya mauaji na ubakaji nchini DRC

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wamefanya "mauaji, ubakaji na uhalifu mwingine wa kivita" mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo tangu mwishoni mwa mwaka 2022, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch (HRW) linashutumu katika ripoti iliyotolewa Jumanne.

HRW inabaini kwamba iliandika kati ya mwezi Novemba 2022 na mwezi Machi 2023 "visa 8 vya mauaji ya kikatli na kesi 14 za ubakaji zilizofanywa na wapiganaji wa M23", na kuongeza kuwa kesi zingine kumi na mbili za mauaji ya kikatili zimehusishwa kundi hili.
HRW inabaini kwamba iliandika kati ya mwezi Novemba 2022 na mwezi Machi 2023 "visa 8 vya mauaji ya kikatli na kesi 14 za ubakaji zilizofanywa na wapiganaji wa M23", na kuongeza kuwa kesi zingine kumi na mbili za mauaji ya kikatili zimehusishwa kundi hili. Β© twitter
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika hili la haki za binadamu, Umoja wa Mataifa unapaswa kuongeza orodha yake ya vikwazo dhidi ya "viongozi wa M23, pamoja na maafisa wa Rwanda" wanaounga mkono kundi hili lenye silaha ambalo lilichukua tena silaha mwishoni mwa 2021.

"Mauaji na ubakaji uliofanywa bila kuchoka na M23 yanatiwa moyo na msaada wa kijeshi ambao makamanda wa Rwanda wanatoa kwa kundi la waasi," amesema ClΓ©mentine de Montjoye, mtafiti wa HRW katika kanda ya Afrika, katika ripoti hiyo.

HRW inabaini kwamba iliandika kati ya mwezi Novemba 2022 na mwezi Machi 2023 "visa 8 vya mauaji ya kikatli na kesi 14 za ubakaji zilizofanywa na wapiganaji wa M23", na kuongeza kuwa kesi zingine kumi na mbili za mauaji ya kikatili zimehusishwa kundi hili. Ripoti hiyo inataja visa ambapo "wapiganaji wa M23 waliwabaka wanawake mbele ya watoto na waume zao".

Mashambulizi ya silaha katika maeneo yenye wakazi wengi ya mkoa wa Kivu Kaskazini yameua na kujeruhi raia, kuharibu miundombinu na kuzidisha mzozo mbaya wa kibinadamu ambao tayari ulikuwa mbaya, ripoti hiyo pia imesema.

Mwishoni mwa mwaka jana, Umoja wa Mataifa kwa upande wake ulishutumu M23 kwa kuwaua zaidi ya raia 170 mwezi Novemba katika kijiji cha Kishishe nchini DRC ambako, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International, makumi ya wanawake pia walibakwa. Viongozi wa M23 walikanusha kuwa vikosi vyao vilifanya uhalifu wowote, linasema Human Rights Watch.

Uungaji mkono wa Rwanda kwa waasi wakati huo umeandikwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa lakini bado unapingwa na Kigali. "Rwanda haitatishwa na kampeni hizi za kupotosha habari na kuvunja nguvu Β juhudi zinazoendelea za amani za kikanda," msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, amejibu siku ya Jumanne huko Kigali, akihojiwa na shirika la habari la AFP.

Ripoti ya HRW inaongeza kuwa makundi yenye silaha yanayopinga kundi la M23, ambayo jeshi la Kongo "linashirikiana nayo", pia yamefanya ubakaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.