Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa wasikitishwa na kuongezeka kwa hali 'tete' mashariki mwa DRC

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (MONUSCO) unaelezea hali ya usalama "inayozidi kuwa tete" mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambako mapigano yanaendelea, katika ujumbe wa mwishoni mwa wiki kwa wafanyakazi wake.

Watu wanatoroka eneo la Masisi karibu na Sake, Februari 7, 2024.
Watu wanatoroka eneo la Masisi karibu na Sake, Februari 7, 2024. AFP - AUBIN MUKONI
Matangazo ya kibiashara

Waasi wa M23 ambao wengi wao ni Watutsi, "umefika kwenye viunga vya kaskazini mwa Sake (karibu kilomita ishirini magharibi mwa Goma, mji mkuu wa Kivu Kaskazini)", unabainisha ujumbe wa Umoja wa Mataifa, ambao unaongeza kuwa "watu wengine wenye silaha wameonekana katika mbuga ya kitaifa ya Virunga na wanatishia kukata barabara ya Goma-Sake."

Ujumbe una maagizo ya kuzuia na kuhama kwa wafanyakazi wake huko Goma, pamoja na kadi ya kukutana sehemu moja ikiwa hali itazorota sana. Goma, ambayo ina wakazi zaidi ya milioni moja na karibu watu milioni moja waliokimbia makazi yao, imezingirwa na waasi wa M23 na vitengo vya jeshi la Rwanda tangu mwezi wa Februari na kuongezeka kwa mapigano. Njia pekee za kutokea ni Ziwa Kivu upande wa kusini na mpaka wa Rwanda upande wa mashariki.

Siku ya Alhamisi, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka India waliotumwa karibu na Sake ili kuzuia kusonga mbele kwa waasi kuelekea Goma walitelekeza ngome zao kwa amri kutoka wakuu wao, kulingana na waraka wa ndani wa MONUSCO ambao shirika la habari la AFP lilipata kopi. "Angalau ngome 3 za ulinzi" zilichukuliwa "na M23 na jeshi la Rwanda" baada ya kutelekezwa na wanajeshi wa India, inabainisha hati hiyo.

Siku ya Jumapili asubuhi, wanamgambo wanaosaidia vikosi vya FARDC (Vikosi vya Wanajeshi wa DRC) waliwafyatulia risasi walinda amani katika viunga vya Sake, "wakiwa na karibu risasi  350 za silaha ndogo na roketi mbili za aina ya RPG", ujumbe huo umeripoti. Siku ya Jumamosi jioni, mlipuko wa guruneti katika kambi ya watu waliokimbia makazi yao, kati ya Goma na Sake, ulisababisha vifo vya watu watano na wengine kadhaa kujeruhiwa, kulingana na vyanzo vya hospitali huko Goma. 

Majibizano ya risasi yaliripotiwa siku ya Jumamosi na Jumapili karibu na Sake na viunga vya magharibi mwa Goma. Raia wawili wanaaminika kuuawa na wengine wawili kujeruhiwa huko Mushaki (kilomita 10 magharibi mwa Sake, katika eneo linalodhibitiwa na M23), kulingana na vyanzo kadhaa vilivyohojiwa kwa simu kutoka Goma. muungano wa serikali unahusishwa na tukio hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.