Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini Afrika Kusini: Mahakama yamruhusu rais wa zamani Zuma kuwa mgombea

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma hatimaye atakuwa mgombea katika uchaguzi wa ubunge uliopangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Mei nchini Afrika Kusini, licha ya hukumu ya kifungo jela mwaka 2021 ambayo ilisababisha uamuzi wa tume ya uchaguzi wa kutomjumuisha kwenye uchaguzi huo.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma mnamo Aprili 17, 2023 katika mahakama ya Pietermaritzburg.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma mnamo Aprili 17, 2023 katika mahakama ya Pietermaritzburg. © Kim Ludbrook / AP
Matangazo ya kibiashara

 

Raia wa Afrika Kusini watapiga kura Mei 29 kulifanya kuwachaguwa wabunge wao wapya, ambao watamchagua rais ajaye. Mwishoni mwa mwezi wa Machi, tume ya uchaguzi (IEC) ilizuia matakwa ya Bw. Zuma, 81, kwa kubatilisha ugombea wake. Chama chake kilichukua hatua za kisheria wiki iliyopita ili uamuzi huu ubatilishwe.

"Rufaa imekubaliwa," iliamua mahakama ya uchaguzi katika uamuzi ambao shirika la habari la AFP limepata kopi, na kuongeza kuwa uamuzi wa tume ya uchaguzi "umebatilishwa". Jacob Zuma ni mgombea katika orodha ya chama kidogo chenye siasa kali kilichoundwa hivi karibuni Umkhonto We Sizwe (MK, "mkuki wa taifa" kwa Kizulu). Aliyekuwa nguzo ya chama cha African National Congress (ANC) madarakani kwa miaka 30, mhusika huyu mkuu katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi alizua mshangao kwa kutangaza mwezi Desemba kwamba anaunga mkono MK.

Chama cha ANC, kilichozama katika biashara na kuwajibika kwa uchumi uliolemewa na ukosefu wa ajira na umaskini unaoongezeka, kinahofia kupoteza wingi wake wa wabunge kwa mara ya kwanza na hivyo kulazimika kuunda serikali ya mseto.

Kwa kutangaza uamuzi wake wa kumtenga Jacob Zuma, tume ya uchaguzi ilikumbusha masharti ya kustahiki yaliyotolewa na Katiba na kusisitiza hasa kwamba mtu aliyehukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 hawezi kuwania katika uchaguzi wa wabunge. Akiwa bado anashitakiwa kwa rushwa, rais huyo wa zamani (2009-2018) alihukumiwa mwaka 2021 hadi miezi 15 jela kwa kosa la kudharau mahakama.

Aliachiliwa kwa msamaha chini ya miezi mitatu baada ya kufungwa kwa sababu za kiafya. Mahakama ya juu zaidi nchini humo iliamua kwamba Bw. Zuma anafaa kurejea gerezani, lakini Rais wa sasa Cyril Ramaphosa hatimaye alipunguza kifungo chake. Katika kikao kilichosikilizwa huko Johannesburg siku ya Jumatatu, wakili wa MK, Dali Mpofu, alidai kuwa "hukumu ya mwisho, kufuatia kusamehewa, ni miezi mitatu".

“Mwachilieni Jacob Zuma”

Akiwa mahakamani, Bw. Zuma alisema mbele ya wafuasi zaidi ya mia moja waliokuwa wakibebelea mabango yaliyoandikwa "Mwacheni Jacob Zuma": "Ikiwa wengi wanataka niwe rais, ni nini kingewazuia?" "Rais Zuma atajitokeza kwenye karatasi za kupigia kura," mmoja wa mabinti wa aliyekuwa mkuu wa nchi, Duduzile Zuma-Sambudla, alichapisha kwenye ukurasa wae wa X siku ya Jumanne akiambatanisha ujumbe wake na picha ya baabke akitabasamu.

Tangu kuanza kwa kampeni, mvutano umekuwa ukiongezeka kati ya ANC na MK. Mwishoni mwa mwezi Machi, mahakama ilikataa ombi la chama tawala kutaka MK iondolewe kwenye orodha ya vyama vilivyosajiliwa kwa uchaguzi huo. Uamuzi bado unasubiriwa baada ya ANC kuwasilisha rufaa nyingine, safari hii ikitaka MK ibadilishe jina na nembo yake. MK ilikuwa wakati wa vita dhidi ya utawala wa kizungu jina la tawi la kijeshi la ANC, ambayo ilishutumu "wizi wa mali miliki na urithi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.