Afrika Kusini: Majaji kuamua iwapo Zuma atawania urais au la
Nairobi – Majaji nchini Afrika Kusini wanatarajiwa kutoa uamuzi iwapo rais wa zamani Jacob Zuma ataruhusiwa kugombea uchaguzi wa mwezi Mei au la, baada ya kuzuiwa na Tume ya Uchaguzi.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Cheza - 00:45
Zuma ambaye alihamia chama cha uMkhonto weSizwe kutoka chama tawala cha ANC, alikosimamishwa uanachama, alikataa rufaa kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi.
Mwezi uliopita, Maafisa wa Tume ya Uchaguzi walieleza kuwa walimzuia Zuma kwa sababu alipatikana na hatia na Mahakama na kuhukumiwa jela, kwa kuidharau Mahakama.
Hata hivyo, Mawakili wake wamedai kuwa hukumu hiyo haimwondolei uhuru wake wa kugomegea uongozi wa nchi yake.
Jumatatu ya wiki hii, Zuma mwenye umri wa miaka 81 akiwa Mahakamani jijini Johannesburg kusikiliza rufaa yake, aliwaambia wafausi wake nje ya Mahakama kuwa, iwapo wananchi wanataka awe rais hakuna anayeweza kumzuia.
Afrika Kusini inatarajiwa kuandaa uchaguzi mkuu tarehe 29 mwezi Mei, unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali katika historia ya nchi hiyo.