Pata taarifa kuu

Zimbabwe yapitisha sarafu mpya kupambana na mfumuko wa bei

Zimbabwe, iliyotumbukia katika mgogoro mkubwa wa kiuchumi kwa takriban miaka ishirini, imeidhinisha sarafu mpya iliyoorodheshwa kwa bei ya dhahabu ili kujaribu kupambana na mfumuko wa bei, Benki Kuu ya nchi hiyo imetangaza siku ya Ijumaa.

Mtu huyu akiwa ameshikilia noti ya dola mbili za Zimbabwe.
Mtu huyu akiwa ameshikilia noti ya dola mbili za Zimbabwe. Getty Images/Bloomberg Creative - Bloomberg Creative Photos
Matangazo ya kibiashara

"Kuanzia leo, benki zitabadilisha salio zinazotumika kwa sasa katika dola za Zimbabwe kuwa sarafu mpya iitwayo Zimbabwe Gold, ZiG," Mkuu wa benki kuu ya taifa ya Zimbabwe, John Mushayavanhu, amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Zimbabwe ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mfumuko wa bei duniani, rasmi 55% mwezi Machi baada ya kufikia kiwango cha tarakimu tatu mwaka jana. Dola ya Zimbabwe ilipoteza karibu 100% ya thamani yake dhidi ya dola ya Marekani katika mwaka uliopita. Ilikuwa ikiuzwa rasmi siku ya Ijumaa kwa takriban dola 30,000 za Zimbabwe kwa dola moja ya Marekani, huku katika soko la magendo dola za Zimbabwe 40,000 ikiuzwa dola moja ya Marekani, kulingana na uchunguzi wa shirika la Zim Price Check.

Mwaka 2008, mfumuko wa bei ulifikia kiwango ambacho benki kuu ilitoa noti ya trilioni ya dola za Zimbabwe. Kisha serikali ililazimika kuachana na fedha za ndani, huku dola ya Marekani ikiwa fedha rasmi. Dola ya Zimbabwe ilifufuliwa mwaka wa 2019. Lakini Wazimbabwe wengi wanapendelea kuendelea kutumia dola ya Marekani, hasa kwa mishahara na katika ulimwengu wa biashara.

Wale wanaolipwa kwa fedha za ndani kwa kawaida hukimbilia kwenye duka la biashara ya sarafu za kigeni siku ya malipo ili kujaribu kupata dola ya Marekani kabla ya kushuka kwa thamani ya sarafu ya ndani. Mbali na mfumuko wa bei, takriban wakazi milioni 15 wameathiriwa na umaskini ulioenea, ukosefu mkubwa wa ajira na uhaba wa chakula, mafuta na hata dawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.