Pata taarifa kuu

Zambia: Shule zafunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu

Shule nchini Zambia zimefunguliwa kwa mara ya kwanza mwaka huu baada ya kucheleweshwa kwa mara kadhaa kutokana na mlipuko wa kipindupindu.

Shule zilicheleweshwa kufunguliwa kutokana na msambao wa ugonjwa wa kipindupindu
Shule zilicheleweshwa kufunguliwa kutokana na msambao wa ugonjwa wa kipindupindu REUTERS - NAMUKOLO SIYUMBWA
Matangazo ya kibiashara

Siku rasimi ya kufunguliwa kwa shule ilichelewesha kwa wiki tano kama sehemu ya hatua zilizochukuliwa kudhibiti msambao wa ugonjwa huo hatari.

Wizara ya elimu kwenye taifa hilo imesema itafanya uchunguzi wa kina kutathmini namana shule zilivyojianda kwa ajili ya ufunguzi.

Hatua hii imekuja wakati huu mamlaka kwenye taifa hilo ikieleza kuwa msambao wa kipindupindu umeanza kupungua.

Karibia watu 500 wameripotiwa kufariki tangu mlipuko huo kuthibitishwa mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Kando na Zambia, nchi za Msumbiji na Zimbabwe pia zimeripoti kuathiriwa na mlipuko wa kipindupindu
Kando na Zambia, nchi za Msumbiji na Zimbabwe pia zimeripoti kuathiriwa na mlipuko wa kipindupindu © Namukolo Siyumbwa / Reuters

Haya yanajiri wakati huu visa zaidi ya 15,000 vya kipindupindu vikiripotiwa, idadi kubwa ya walioathirika ikiwa ni watoto.

Zambia imekuwa ikikabiliwa na mlipuko wa kipindupindu kwa miaka kadhaa, maambukizi ya hivi punde yakielezwa kuwa mbaya zaidi katika kipindi cha miaka 20 kwa mujibu wa serikali.

Nchi za Zimbabwe na Msumbiji nazo pia zimeripoti maambukizi ya ugonjwa huo, vifo pia vikiripotiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.