Pata taarifa kuu

Ethiopia: HRW yataka uchunguzi wa UN kuhusu mauaji ya raia yaliyotekelezwa na jeshi Amhara

Shirika lisilo la kiserikali la Human Rights Watch (HRW) limetoa wito leo Alhamisi kwa Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya "dazeni kadhaa" ya raia yaliyofanywa na jeshi la Ethiopia mwishoni mwa mwezi Januari katika eneo la Merawi, katika jimbo la kikanda la Amhara lialokumbwa machafuko.

Mji wa Merawi, Ethiopia, kweye ramani.
Mji wa Merawi, Ethiopia, kweye ramani. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Katikati ya mwezi wa Februari, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Ethiopia (EHRC), taasisi ya umma inayojitegemea kisheria, ilibaini kwamba takriban wakazi 45 wa Merawi waliuawa Januari 29 na vikosi vya serikali baada ya mapigano na wanamgambo wa eneo la Fano, idadi ambayo huenda ikawa juu.

Kulingana na ushuhuda uliokusanywa na HRW, baada ya kuondoka kwa Fano kutoka Merawi, eneo lililoko takriban kilomita 30 kusini mwa mji mkuu wa mkoa wa Bahir Dar, wanajeshi wa Ethiopia waliwashambulia wakazi kwa "saa sita", na kuua wanamume na wanawake "mitaani" au wakati wa upekuzi” na “kupora na kuharibu mali ya raia.” shirika hili la kimataifa lisilo la kiserikali linasema "halijaweza kubainisha jumla ya idadi ya raia waliouawa Merawi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.