Pata taarifa kuu

Spika wa Bunge la Madagascar avuliwa wadhifa wake

Rais wa Bunge la taifa la Madagascar, aliyekuwa akiungwa mkono na mkuu wa nchi Andry Rajoelina ambaye alikuwa akiikosoa sana serikali wakati wa uchaguzi wa rais mwezi Novemba, amevuliwa wadhifa wake, kulingana na vyanzo kadhaa, vikinukuliwa na shirika la habari la AFP.

Christine Razanamahasoa, ambaye sasa anaonekana kama kiongozi mkuu wa upinzani, aliomba haswa mwanzoni mwa mwezi Novemba, wiki moja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, "kusimamishwa kwa uchaguzi", katika mazingira magumu ya maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ambao ulishutumu njama inayolenga kumpatia rais anayemaliza muda wake muhula wa pili.
Christine Razanamahasoa, ambaye sasa anaonekana kama kiongozi mkuu wa upinzani, aliomba haswa mwanzoni mwa mwezi Novemba, wiki moja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, "kusimamishwa kwa uchaguzi", katika mazingira magumu ya maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ambao ulishutumu njama inayolenga kumpatia rais anayemaliza muda wake muhula wa pili. Capture d'écran youtube
Matangazo ya kibiashara

Katika uamuzi uliotolewa hadharani Alhamisi jioni, Mahakama Kuu ya Kikatiba ilimvua Christine Razanamahasoa, 72, wadhifa wake kama mbunge, ikizingatiwa kuwa "amekiuka kabisa" mwenendo wa chama chake, na kwa sababu ya wadhifa wake kama spika wa Bunge.

Anakumbusha kwamba "vitendo vya upande mmoja kinyume na maadili na ahadi" za kundi lake la kisiasa "ni ukiukwaji wa wazi wa kifungu cha 72 cha Katiba" kinachosema kwamba mbunge "lazima aheshimu safu ya maadili ya kundi lake la bunge na kwamba hawezi kubadilisha kundi lake la kisiasa na kujiunga na kundi jipya, zaidi ya lile ambalo alichaguliwa kwa niaba yake.

Christine Razanamahasoa, ambaye sasa anaonekana kama kiongozi mkuu wa upinzani, aliomba haswa mwanzoni mwa mwezi Novemba, wiki moja kabla ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais, "kusimamishwa kwa uchaguzi", katika mazingira magumu ya maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ambao ulishutumu njama inayolenga kumpatia rais anayemaliza muda wake muhula wa pili. "Masharti ya uchaguzi wa amani na wa kuaminika unaokubaliwa na wote hayatimizwi," alisema wakati huo.

Tayari mwezi Oktoba, alitangaza: "Nchi yetu iko katika hali mbaya, watu wetu wanateseka, na sisi ndio sababu ya kushindwa huku. Tuko katika hali mbaya." Christine Razanamahasoa, jaji wa zamani, alikuwa Waziri wa Sheria kisha spika wa Bunge kwa muda mfupi mnamo 2014, na hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi hii, kabla ya kuchaguliwa tena mnamo mwaka 2019.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.