Pata taarifa kuu

Madagascar: Rais Rajoelina anazidi kupokea shinikizo kutuliza joto la kisiasa

Nairobi – Rais wa Madagascar Andry Rajoelina ameendelea kupokea shinikizo kutoka kwa jamii ya kimataifa kutuliza joto na kisiasa na wasiwasi unaolikumba taifa hilo baada ya ushindi wake kuidhinishwa na mahakama, Marekani na EU zikiongoza wito huo.

Mabalozi wa EU na Marekani katika taarifa yao, wametaka Rajoelina kuchukua hatua za kurejesha imani pamoja na kufanyika kwa mazungumzo
Mabalozi wa EU na Marekani katika taarifa yao, wametaka Rajoelina kuchukua hatua za kurejesha imani pamoja na kufanyika kwa mazungumzo AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kikatiba kwenye taifa hilo imethibitisha ushindi wa rais Rajoelina katika uchaguzi wa urais wa tarehe 16 mwezi Novemba.

Upinzani ulikuwa umesema uchaguzi huo haukufanyika kwa uhuru na haki na kulikuwepo na udaganyifu, madai ambayo mahakama imetuipilia mbali.

Kwa mujibu mahakama, rais Rajoelina alipata asilimia 59 ya kura katika uchaguzi ambao asilimia 46 ya wapiga kura walishiriki licha ya wapinzani kususia.

Wagombea wa upinzani walisusia kushiriki katika uchaguzi huo
Wagombea wa upinzani walisusia kushiriki katika uchaguzi huo AFP - MAMYRAEL

Baada ya kuidhinishwa na mahakama, Rajoelina, ameutaja ushindi wake kama mkubwa na kwamba hatoruhusu ukosoaji ambao amesema ni wa kumboa nchi na kwamba lazima uamuzi wa wapiga kura uheshimiwe.

Licha ya uamuzi wa mahakama, wanasiasa 11 wa upinzani wamesisitiza kuwa hawatambui matokeo ya uchaguzi huo na kwamba msimamo wao ni kuwa zoezi hilo lilikumbwa na udaganyifu.

Licha ya mahakama kuidhinisha ushindi wa Andry Rajoelina, wanasiasa wa upinzani wanasema hawatambui ushindi wake .
Licha ya mahakama kuidhinisha ushindi wa Andry Rajoelina, wanasiasa wa upinzani wanasema hawatambui ushindi wake . © Photos AFP - Montage RFI

Mabalozi wa EU na Marekani katika taarifa yao, wametaka Rajoelina kuchukua hatua za kurejesha imani pamoja na kufanyika kwa mazungumzo.

Rajoelina aliingia madarakani kwa mara ya kwanza mwaka wa 2009 kufuatia mapinduzi ya kijeshi dhidi ya matangulizi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.