Pata taarifa kuu

Takriban watu wanne wafariki kwa moto uliyozuka kwenye kiwanda cha mafuta Gabon

Takriban watu wanne walifariki Jumatano, na mmoja wa tano hajulikani aliko, kutokana na moto uliyozuka kwenye katika kiwanda cha kampuni ya mafuta ya Mfaransa mwenye asili ya Uingereza ya Perenco Oil & Gas katika pwani ya Gabon, Wizara ya Mafuta na Gesi imetangaza siku ya Alhamisi.

Ajali hii" ni "janga kubwa zaidi katika historia ya uchimbaji wa mafuta katika nchi yetu", amesema Marcel Abéké, Waziri wa Mafuta, katika taarifa kwa vyombo vya habari. (picha ya kielelezo)
Ajali hii" ni "janga kubwa zaidi katika historia ya uchimbaji wa mafuta katika nchi yetu", amesema Marcel Abéké, Waziri wa Mafuta, katika taarifa kwa vyombo vya habari. (picha ya kielelezo) © AP
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa usiku, Perenco ilitangaza kuwa watu watano hawajulikani waliko. Moto huo ulizuka katikati ya alasiri kwenye jukwaa liitwalo Becuna, lililo karibu na kituo cha mafuta cha Tchatamba, kwenye pwani ya kusini mashariki mwa Gabon.

"Tunasikitishwa na vifo vya watu wanne, mtu wa tano hajulikani aliko," imesema Wizara ya Mafuta na Gesi imetangaza katika taarifa kwa vyombo vya habari ikibainisha kuwa "watu saba kati ya kumi na wawili waliokuwa kiwanda hiki wakati wa ajali waliweza kuhamishwa".

"Eneo lililindwa, moto ulidhibitiwa na wafanyikazi wote waliokuwepo kwenye ndani ya kiwanda ambao hawakujeruhiwa walihamishwa," Perenco imethibitisha siku ya Alhamisi asubuhi, pia ikiwataja majeruhi wawili. Mmoja wa majeruhi wawili aliungua vibaya, kulingana na wizara.

"Ajali hii" ni "janga kubwa zaidi katika historia ya uchimbaji wa mafuta katika nchi yetu", amesema Marcel Abéké, Waziri wa Mafuta, katika taarifa kwa vyombo vya habari, akibaini kwamba "mwanga utatolewa juu ya hali iliyosababisha ajali hii na mafunzo ambayo watu wanatakiwa kujifunza kutokana na tukio hilo. "Ajali ilitokea wakati wa operesheni ya workover (kuingia ndani ya kisima), inabainisha taarifa kwa vyombo vya habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.