Pata taarifa kuu

Gabon: Utawala wa Jenerali Oligui Nguema wakabiliwa na ukosoaji mkubwa

Miezi sita baada ya mapinduzi yaliyompindua Rais Ali Bongo Ondimba, Jenerali Brice Oligui Nguema ana umaarufu mkubwa nchini Gabon, lakini ukosoaji wa kwanza unaibuka kuhusu utawala unaochukuliwa kuwa wa kimabavu na wapinzani wake na ambao unachelewa kufikia malengo yake ya "bora kuishi".

Jenerali Oligui, 48, alichaguliwa kwa ushindi kama rais wa mpito, na kuahidi kurejesha mamlaka kwa raia kupitia uchaguzi, ndani ya muda uliowekwa baadaye kuwa miaka miwili.
Jenerali Oligui, 48, alichaguliwa kwa ushindi kama rais wa mpito, na kuahidi kurejesha mamlaka kwa raia kupitia uchaguzi, ndani ya muda uliowekwa baadaye kuwa miaka miwili. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi hao ambao walitangaza, bila kumwaga damu, Agosti 30 "mwisho wa utawala wa Bongo", saa moja baada ya tangazo la kuchaguliwa kwake tena ambapo jeshi lilichukulia uchaguzi huo kuwa wa udanganyifu. wakati huo jeshi lilipata uungwaji mkono mkubwa kote nchini. Jenerali Oligui, 48, alichaguliwa kwa ushindi kama rais wa mpito, na kuahidi kurejesha mamlaka kwa raia kupitia uchaguzi, ndani ya muda uliowekwa baadaye kuwa miaka miwili.

Kwa zaidi ya miaka 55, familia ya Bongo - baba, Omar, nguzo ya "Françafrique" kutoka mwaka 1967 hadi mwaka 2009, kisha mtoto Ali - alitawala bila kugawana madarakakatika nchi hii ndogo ya Afrika ya Kati, tajiri kwa mafuta yake, lakini chini ya nira ya wasomi wanaoshutumiwa na wapinzani wake kwa "ufisadi mkubwa" na "utawala mbaya".

Jenerali Oligui "alifika wakati ambapo Wagabon hawakuwa tena na uwezo wa kufanya maamuzi yoyote", anasema François Ndong Obiang, kiongozi wa zamani wa upinzani leo makamu wa spika wa Bunge la mpito la taifa, ambalo wabunge wake wote waliteuliwa na kiongozi mpya.

Nchi hiyo, ambayo ina wakazi milioni 2.3, ambao nusu yao ni chini ya umri wa miaka 20, "ilikuwa katika hali mbaya katika suala la miundombinu, elimu, afya", na Jenerali Oligui, kulingana na François Ndong, alionekana kama "mwokozi".

"Kuiinua nchi"

Nchi hiyo ni mojawapo ya nchi tajiri zaidi barani Afrika kwa kila mwananchi lakini mmoja kati ya wakazi watatu anaishi chini ya mstari wa umaskini, kwa chini ya euro mbili kwa siku, kulingana na Benki ya Dunia.

Kwa watu wa Gabon ambao bado wanasubiri barabara na shule katika hali nzuri, au wanaoishi bila maji au umeme wakati mwingine katikati ya mji mkuu, Kamati ya Mpito na Marejesho ya Taasisi (CTRI), iliyoundwa na majenerali, inaahidi "kunyoosha nchi kiuchumi" na "kupambana na gharama kubwa ya maisha".

Hasa kupitia malipo ya malimbikizo mengi ya pensheni, ujenzi wa barabara na hospitali, kurudi kwa ufadhili wa shule na ahadi zingine nyingi za "maisha bora". Lakini hazina ya serikali imesalia tupu. Katikati ya mwezi waFebruari, licha ya "hali ngumu ya bajeti", Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) hata hivyo lilitambua CTRI kwa "juhudi zilizolenga kuimarisha uwazi na usimamizi wa fedha za umma". Taasisi hiyo, hata hivyo, inaonya kuhusu "kushuka kwa uzalishaji wa mafuta, kudorora kwa mapato ya kila mtu" na "kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira".

CTRI iliwateua majenerali katika uongozi wa miji mikuu na askari wengi huchanganyika na raia ndani ya taasisi za uongozi. Lakini Jenerali Oligui anakosolewa kwa kuwaacha kwa kiasi kikubwa viongozi wa utawala mkongwe madarakani, hasa kutoka chama cha Gabon Democratic Party (PDG) ya Omar na Ali Bongo.

"Sura za utawala wa mpito ni sura zinazojulikana," anasisitiza Joanna Boussamba, msemaji wa shirika la uchunguzi wa utawala wa umma Copil Citoyen, ambaye anasikitishwa na "ujumbe wa kutokujali" na sehemu ndogo iliyoachwa kwa mashirika ya kiraia. "Mabadiliko yanajumuisha, lazima yazingatie kila mtu, hata Mkurugenzi Mkuu," anajibu makamu wa spika wa Bunge la taifa. Lakini "ni watu wanane tu waliokamatwa," anasema Bi Boussamba.

Anarejelea msafara wa Ali Bongo, mkewe Sylvia na mtoto wao wa kiume Noureddin, waliowekwa kizuizini tangu Agosti 30, wakituhumiwa haswa kwa ubadhirifu mkubwa wa pesa za umma na kughushi saini ya rais wa zamani. Mkuu wa serikali aliyepinduliwa kwa upande wake anashikilwa katika makazi yake ya kifahari huko Libreville.

"Ubabe"

Mamlaka hiyo mpya pia inashutumiwa na upinzani kwa ubabe. Kwa mfano, serikali imeshikilia kwa muda wa miezi sita, bila kutoa maelezo hata kidogo, marufuku kali ya kutotoka nje kuanzia saa 6:00 usiku hadi saa 11:00 asubuhi, iliyowekwa awali na utawala wa Bongo jioni ya uchaguzi wa urais wa Agosti 26, 2023.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.