Pata taarifa kuu

Rais wa mpito wa Gabon kuzuru Kongo

Rais wa mpito wa Gabon, Jenerali Brice Oligui Nguema, atakutana na mwenzake kutoka nchi jirani ya Kongo, Denis Sassou Nguesso, siku ya Jumapili, Télesphore Obame Ngomo, mshauri maalum wa mkuu wa nchi wa Gabon, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Alhamisi.

Jenerali Brice Oligui Nguema (wa pili kutoka kushoto) akikagua wanajeshi kabla ya gwaride la kijeshi, mjini Libreville, Septemba 4, 2023.
Jenerali Brice Oligui Nguema (wa pili kutoka kushoto) akikagua wanajeshi kabla ya gwaride la kijeshi, mjini Libreville, Septemba 4, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Rais wa mpito atasafiri siku ya Jumapili kwa ziara huko Oyo (katikati ya Kongo) kama sehemu ya mkutano wa faragha" na mwenzake Bw. Sassou Nguesso, ametangaza Bw. Ngomo, akiongeza kuwa "ziara nyingine zimepangwa" hivi karibuni katika kanda, bila maelezo zaidi.

Siku ya Jumanne, wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa Ofisi ya rais wa Jamhuri ya Gabon (SGPR), Guy Rossatanga-Rignault, N'Djamena, mji mkuu wa Chad, "kanuni ya ziara ya Bw. Oligui ilijadiliwa, lakini hakuna tarehe iliyotangazwa,” Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad Mahamat Saleh Annadif ameliambia shirika la habari la AFP.

Uhusiano kati ya Kongo ya Denis Sassou Nguesso, ambaye ana takriban miaka 40 madarakani, na Gabon ya Ali Bongo Ondimba, ulikuwa na mvutano mkubwa. Hii ni zira ya pili ya Bw. Oligui nje ya nchi tangu jeshi lilipompindua Ali Bongo, ambaye alikuwa madarakani kwa miaka 14. Babake, Omar Bongo Ondimba, aliyefariki mwaka wa 2009, alikuwa ametawala nchi hiyo kwa mkono wa chuma kwa zaidi ya miaka 40.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.