Pata taarifa kuu

Kipindi cha mpito chaibua maswali kwa utawala wa kijeshi Gabon

Nchini Gabon, mabadiliko yamekuwa yakiendelea tangu mapinduzi ya kijeshi mwishoni mwa Agosti ambayo yalimpindua Rais Bongo. Kunasubiriwa hasa uteuzi wa wabunge katika Bunge na Seneti ya mpito. Muda wa mpito haujulikani. Jenerali Oligui Nguema ambaye alichukua mamlaka alisema kuwa ni juu ya wadau wote kuamua ni muda gani kipindi cha mpito kitachukuwa. Mapendekezo kadhaa yapo mezani kwa sasa.

Jenerali Brice Oligui Nguema wakati wa kuapishwa kwake kama rais wa mpito, mjini Libreville, Septemba 4, 2023.
Jenerali Brice Oligui Nguema wakati wa kuapishwa kwake kama rais wa mpito, mjini Libreville, Septemba 4, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kipindi cha mpito cha miaka miwili ni pendekezo ambalo hutolewa na wengi nchini Gabaon. Waziri Mkuu, Raymond Ndong Sima, anaona hili kama "lengo la busara". Hata hivyo, muda wa mwisho utaamuliwa mwishoni mwa kongamano kuu la kitaifa. "Sio juu ya Bunge, wala jeshi kuchagua. Mkutano huo utaanzisha ratiba ambayo itaidhinishwa na Baraza la Bunge na Bunge la Seneti,” amesema mmoja wa maafisa waandamizi wa utawala wa kijeshi.

Mashirika ya kiraia kwanza yalipendekeza miezi sita hadi mwaka. "Ilikuwa ni kuonyesha kwamba jeshi halingeweza kusalia madarakani milele," anasema Jaji Lekogo wa Copil Citoyen. Lakini kutokana na miradi inayoendelea, mashirika hayo hatimaye yamependekeza kati ya miezi 18 hadi 24. "Lazima tuvunje mamlaka iliyowekwa kwa miaka 60, kujenga upya demokrasia, kupigia kura sheria mpya na Katiba ya nchi kabla ya kujiandaa kwa uchaguzi," anabaini George Mpaga, kutoka shirika la ROLBG, kuelezea majitaji ya wakati.

Lakini kwenda zaidi ya miaka miwili kunaweza kuleta shida. "Utawala wa mpito haupo kutatua masuala yote muhimu. Hili lazima lifikiwe na mamlaka mpya iliyochaguliwa,” anasema Justine Lekogo.

Kwa upande wa kisiasa, Alexandre Barro Chambrier, kiongozi wa RPM, pia amependekeza miaka miwili. Ni wakati wa kuirejesha Gabon kwenye mstari. Lakini hatupaswi kuonja raha za madaraka,” alitangaza.

Kuhusu muungano mkuu wa Alternance 2023, unasubiri Mkutano huo kupendekeza muda. Lakini afisa mmoja anabaini kwamba "kutokana na mageuzi yanayotakiwa kufanywa, ndani ya mfumo ulio imara zaidi, si rahisi," anasema. Hata hivyo, "hatupaswi kuzidi theluthi mbili ya muhula wa miaka mitano", kulingana na afisa huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.