Pata taarifa kuu
SIASA-MARIDHIANO

Gabon: Jean Ping atangaza kuwa 'tayari kufanya kazi' na viongozi wapya

Nchini Gabon, hali ya utulivu ya kisiasa inaendelea baada ya mapinduzi ya Agosti 30. Kiongozi wa nchi hiyo aliyechukuwa malaka kupitia mapinduzi ya kijeshi, Jenerali Brice Clotaire Oligui Nguema amekutana na Jean Ping, mpinzani na mkosoaji mkubwa wa Ali Bongo, rais aliyepinduliwa madarakani.

Jean Ping mnamo Julai 13, 2023.
Jean Ping mnamo Julai 13, 2023. © RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Libreville, Yves-Laurent Goma

Mkutano huo ulifanyika kwa awamu mbili. Kwanza kati ya Jean Ping, wasaidizi wake na rais wa mpito Brice Clotaire Oligui Nguema akiwa na wajumbe wa baraza lake la mawaziri.

Kisha Jean Ping na kiongozi mpya wa Gabon Brice Clotaire Oligui Nguema walikutana ana kwa ana kwa mazungumzo. Mwishoni mwa mazungumzo yao, Jean Ping, mwenye aliondoka huku akitabasamu, na kubadilisha msimamo papo hapo. "Nimepewa heshima yangu kama mmoja wa watu muhimu katika nchi hii na nimefurahi kuwa na mazungumzo na kiongozi mpya. Nafikiri - narudia tena - kwamba rais wa Jamhuri, Mheshimiwa Brice Oligui Nguema, amefanya kazi kubwa ya kusafisha nchi. Kila mtu anamtambua, kila mtu anampenda na sisi tupo, tayari kufanya kazi, tayari kufanya naye kazi na tayari kuchukua majukumu yetu, ikiwa tutaombwa tuyachukue tunavyoamini! "

Kwa miaka saba iliyopita, Jean Ping ameishi katika kifungo cha nyumbani katika makazi yake katika eneo la Charbonnages. Amekuwa akiendelea kudai ushindi wake katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2016 ambao anaamini kuwa uliibiwa na Ali Bongo. Pasipoti yake aliyonyang'anywa alirejeshewa miezi miwili kabla ya uchaguzi uliopita wa urais. Akiwa na umri wa miaka 80, mwanadiplomasia huyo anasema yuko tayari kuitumikia tena nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.