Pata taarifa kuu

Gabon: Hali ya mahabusu ni mbaya sana katika magereza  na vituo vya polisi

Nairobi – Kamati ya Umoja wa Mataifa inayozuia visa vya mateso ya binadamu katika ripoti yake imesema, hali ya mahabusu ni mbaya sana katika Magereza  na vituo vya polisi nchini Gabon.

Hali hii inawafanya wafungwa hao kuhukumiwa hata kabla ya kesi zao kuanza au kutamatika kwa mujibu wa Katamati hiyo ya Umoja wa Mataifa
Hali hii inawafanya wafungwa hao kuhukumiwa hata kabla ya kesi zao kuanza au kutamatika kwa mujibu wa Katamati hiyo ya Umoja wa Mataifa AFP - WILS YANICK MANIENGUI
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Kamati hiyo inasema, haki za msingi za wafungwa zinakiukwa katika taifa hilo la Afrika ya Kati na inataka serikali nchini humo kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha hali hiyo.

Abdallah Ounnir, aliongoza ujumbe wa watalaam wa Kamati hiyo na kuzur Magereza nchii Gabon kati ya tarehe 10 hadi 16 na kuripoti mrundikano wa waafungwa na mazingira anayosema sio ya kiutu kwa binadamu kuzuiwa.

Aidha, imebainika kuwa sababbu kubwa inayosababisha mrundikano huo wa wafungwa ni kuzuiwa kwa muda mrefu kabla ya kuanza kwa kesi zinazowakabili.

Hali hii inawafanya wafungwa hao kuhukumiwa hata kabla ya kesi zao kuanza au kutamatika kwa mujibu wa Katamati hiyo ya Umoja wa Mataifa.

Hii sio mara ya kwa Gabon kutajwa kukiuka haki za wafungwa baada ya ripoti nyingine kama hii kutolewa mwaka 2013 na mapendekezo kutolewa kwa serikali kuimarisha hali ya Magereza lakini miaka zaidi ya 10 baadaye, hakuna kilichofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.