Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Laurent Gbagbo kupeperusha bendera ya PPA-CI katika uchaguzi wa urais wa 2025 Côte d'Ivoire

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire, Laurent Gbagbo, amekubali kuwa mgombea wa chama cha African People's Party - Côte d'Ivoire (PPA-CI) katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2025, amesema msemaji wake, Katinan Koné, baada ya kikao cha kamati kuu ya chama.

Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan mnamo Agosti 22, 2023.
Rais wa zamani wa Côte d'Ivoire Laurent Gbagbo akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan mnamo Agosti 22, 2023. AFP - SIA KAMBOU
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2025. Rais Alassane Ouattara, ambaye alichaguliwa tena mwaka wa 2020, bado hajafafanua iwapo atawania tena urais au la.

Mgombea mwingine anayewezekana ni Tidjane Thiam, mtendaji mkuu wa zamani wa benki ya Uswizi Credit Suisse, ambaye mwezi Desemba aliteuliwa kuwa kiongozi wa chama cha PDCI, moja ya vyama vikuu vya upinzani nchini Côte d'Ivoire, ingawa chama hiki bado hakijamteua rasmi mgombea wake.

Bw. Gbagbo, rais wa Côte d'Ivoire kuanzia mwaka 2000 hadi 2011, alizindua Chama cha African People's Party - Côte d'Ivoire mnamo mwaka 2021, kufuatia kuachiliwa kwake kwa uhalifu wa kivita na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.