Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Côte d'Ivoire: Chama cha Gbagbo chashutumu 'upungufu' kwenye orodha ya uchaguzi

Chama cha PPA-CI, chama cha Laurent Gbagbo, kinashtumu, 'ukiukwaji na udanganyifu' kwenye orodha ya uchaguzi, ambapo rais wa zamani wa Côte d'Ivoire bado ameondolewa kwenye orodha ya wagombea, miezi mitatu kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa magavana.

Mkurugenzi katika ofisi ya Laurent Gbagbo, Wakili Habiba Touré, mwenekiti wa "Safe", chombo kilichoundwa na PPA-CI kupambana dhidi ya udanganyifu katika uchaguzi, amebainisha katika mkutano na waandishi wa habari kwamba timu zake zilionysha "upungufu" kwenye orodha ya uchaguzi, Mei 30, 2023, mjini Abidjan.
Mkurugenzi katika ofisi ya Laurent Gbagbo, Wakili Habiba Touré, mwenekiti wa "Safe", chombo kilichoundwa na PPA-CI kupambana dhidi ya udanganyifu katika uchaguzi, amebainisha katika mkutano na waandishi wa habari kwamba timu zake zilionysha "upungufu" kwenye orodha ya uchaguzi, Mei 30, 2023, mjini Abidjan. © Marine Jeannin/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Abidjan siku ya Jumanne, Habiba Touré, mwenyekiti wa "Safe", chombo kilichoundwa na chama cha PPA-CI kupambana dhidi ya udanganyifu katika uchaguzi, alibaini kwamba orodha hiyo "imejaa dosari na udanganyifu". Bi. Touré, pia mkurugenzi katika ofisi ya Laurent Gbagbo, kwanza alibainisha, kwa ushuhuda wa picha za skrini za orodha hiyo, kwamba watoto 'kati ya miaka 3 na 14' wameorodheshwa.

Akihojiwa na mwandishi wetu wa habari huko Abidjan, Marine Jeannin, alibainisha majina ya watu "waliozaliwa katika karne ya 19" kabla ya kutaja kesi ya watu waliokufa, lakini bado wamesajiliwa. "Katika uchunguzi wa orodha, inaweza kuzingatiwa kuwa watoto wadogo wameorodheshwa kwenye orodha ya wapiga kura. Watu waliozaliwa katika karne ya 19, na ambao mtu anaweza kutilia shaka kwamba bado wako hai, hata hivyo wameorodheshwa vyema kwenye orodha ya wapiga kura. Watu waliofariki wameorodheshwa kwenye orodha ya wapiga kura. "

Hatimaye, Bi. Touré alisikitishwa na ukweli kwamba watu kadhaa waliopatikana na hatia ya uhalifu, na kwa hivyo wanaodaiwa kunyimwa haki zao za kiraia na kisiasa, bado wamesajiliwa kwenye orodha ya wapiga kura. "Watu waliohukumiwa kwa uhalifu wako kwenye orodha ya wapiga kura. Watu wenye nambari mbili au hata tatu za kipekee, nambari maarufu inayodaiwa kuwa ya kipekee, kuna wale ambao wana mbili au tatu, na wako kwenye orodha ya wapiga kura. Watu hawa wote, nakala zote hizi zinaweza kusajiliwa kwenye orodha ya wapiga kura… lakini si Rais Laurent Gbagbo. "

Akihojiwa na RFI siku ya Jumanne, msemaji wa Tume Huru ya Uchaguzi (CEI) amekataa kutoa maoni yake na kuashiria kuwa IEC ilikuwa ikisubiri kupokea malalamishi hayo. Rufaa zinaweza kuwasilishwa kuanzia Juni 1 hadi 10.

Mnamo Mei 20, tume ilichapisha orodha ya uchaguzi bila jina la Laurent Gbagbo, ikionyesha kuwa alikuwa mmoja wa watu 11,000 waliopokonywa haki zao za kiraia na kisiasa kufuatia kutiwa hatiani. Ingawa aliachiliwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC, kwa uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa wakati wa mgogoro wa umwagaji damu baada ya uchaguzi wa 2010-2011, bado yuko chini ya kifungo cha miaka 20 jela nchini Côte d'Ivoire kwa "wizi" wa Benki Kuu ya mataifa ya Afrika Magharibi (BCEAO) mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.