Pata taarifa kuu
JAMII-NDOA

Côte d’Ivoire: Laurent Gbagbo na Simone Ehivet Gbagbo wameachana rasmi

Talaka kati ya Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Gbagbo na mkewe Simone, iliyoombwa baada ya kurejea Abidjan mnamo Juni 2021 na Mkuu wa zamani wa Nchi baada ya kuachiliwa kwake na Mahakama ya kimataifa, ilitangazwa rasmi Juni 29, 2023, inasema taarifa kutoka kwa manasheria wa Simone Gbagbo.

Laurent Gbagbo na Simone Ehivet Gbagbo.
Laurent Gbagbo na Simone Ehivet Gbagbo. © Photos AFP - Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne

Nchini Côte d'Ivoire, mahakama ilitangaza siku ya Alhamisi talaka kati ya Simone Ehivet Gbagbo na Laurent Gbagbo, kulingana na Wakili Rodrigue Dadjé, mwanasheria wa mke wa rais wa zamani.

Hapo awali, ombi hili lilitoka kwa rais wa zamani wa nchi (2000-2011), ambaye, alichukua hatua hii, aliporejea Abidjan mnamo mwezi Juni 2021.

Kwa talaka imetagazwa rasmi. "Talaka imetangazwa kwa kosa la kipekee la Bw. Laurent Gbagbo, kwa uzinzi wenye sifa mbaya, kutelekeza ndoa yake na matusi makubwa dhidi ya Bi. Simone", inathibitisha taarifa kutoka mwanasheria wa mke wa rais wa zamani wa Côte d'Ivoire.

Hati hii haitaji athari za kifedha za talaka hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.