Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Côte d'Ivoire: Laurent Gbagbo hataweza kupiga kura kwa uchaguzi ujao

Chama chake cha kisiasa, African Peoples' Party-Côte d'Ivoire (PPA-CI), hakikuwasilisha rufaa ya mwisho kwenye mahakama ya utawala.

Rais wa zamani Laurent Gbagbo akizungumza karibu na ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi, CEI, huko Abidjan, Juni 8, 2023.
Rais wa zamani Laurent Gbagbo akizungumza karibu na ofisi za Tume Huru ya Uchaguzi, CEI, huko Abidjan, Juni 8, 2023. AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Abidjan, François Hume-Ferkatadji

PPA-CI ilikuwa na siku tatu kuanzia Jumatatu, Juni 26 kuwasilisha rufaa ya pili katika mahakama ya utawala. Utaratibu huu wa kisheria haukuzinduliwa. Kwa miezi kadhaa, chama hicho kimekuwa kikiomba kurejeshwa kwa Laurent Gbagbo kwenye orodha ya wapiga kura. "Hatutafanya ombi sawa, kwa majaji wale wale", anaelezea Justin Koné Katinan, msemaji wa chama.

Mwishoni mwa mwezi Juni, Tume Huru ya Uchaguzi ilikataa ombi hili.

Akiwa ameachiliwa na ICC kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu uliotendwa wakati wa mgogoro wa baada ya uchaguzi wa 2010-2011, rais huyo wa zamani wa Côte d'Ivoire bado yuko chini ya kifungo cha miaka 20 jela nchini Côte d'Ivoire kwa kesi  ya wizi katika benki ya Mataifa ya Afrika Magharibi, BCEAO, mwaka 2011. Hukumu ambayo Laurent Gbagbo "anafutilia mbali", alikumbusha hivi karibuni.

Akiwa amesamehewa na urais, lakini bado hajafutiwa kosa hilo, kwa hivyo ataendelea kunyimwa haki zake za kiraia.

Wafuasi wa Laurent Gbagbo bado wanaweza kutumaini kuwa kiongozi wa PPA-CI atasimama katika uchaguzi ujao wa rais. Hakika, marekebisho mapya ya orodha ya wapiga kura yamepangwa kabla ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa chama chake, Laurent Gbagbo "anachukulia kutosajiliwa huku kama mbinu ya kisiasa inayolenga kumweka nje ya maisha ya kisiasa", hata hivyo "hajaathiriwa na hali hiyo", inabainisha taarifa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.