Pata taarifa kuu

Mahakama ya Tunisia yabatilisha kifungo cha miaka 5 jela cha mwandishi wa habari

Mahakama Kuu nchini Tunisia siku ya Jumatano imebatilisha hukumu ya mwandishi wa habari kifungo cha miaka mitano gerezani, na hivyo kufungua njia ya kuachiliwa kwake akisubiri kusikilizwa kwa kesi mpya, wakili wake amelimbia shirika la habari la AFP.

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na kimataifa yametoa wito kadhaa wa kuachiliwa kwake, na kushutumu kifungo chake cha miaka mitano jela kama "mbinu isiyofaa ya kutaka kunyamanzisha vyombo vya habari" na "kizuizi kikubwa kwa mfumo wa mahakama".
Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na kimataifa yametoa wito kadhaa wa kuachiliwa kwake, na kushutumu kifungo chake cha miaka mitano jela kama "mbinu isiyofaa ya kutaka kunyamanzisha vyombo vya habari" na "kizuizi kikubwa kwa mfumo wa mahakama". © FETHI BELAID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Khalifa Guesmi, mwandishi wa kituo cha Mosaïque FM,  Radio maarufu nchini Tunisia, alihukumiwa mwezi Novemba 2023 kifungo cha mwaka mmoja jela, kifungo kiliongezeka hadi miaka mitano katika ngazi ya rufaa, kwa kufichua habari kuhusu idara za usalama.

Mahakama Kuu "imebatilisha hukumu ya miaka mitano na kuamuru ipitiwe upya baada ya kukata rufaa", mwaasheria wake, WAkili Rahal Jallali, ameliambia shirika la habari la AFP. Kulingana nna wakili huyo, Khalifa Guesmi anapaswa kuachiliwa Jumatano jioni au Alhamisi asubuhi.

Mwanahabari huyo anaendelea kufunguliwa mashitaka kulingana na wakili wake, chini ya kifungu cha 34 cha sheria ya kupambana na ugaidi ambayo "inaadhibu kifungo cha miaka kumi hadi ishirini" mtu yeyote anayechapisha habari "kwa faida ya shirika au makubaliano ya kigaidi".

Akiwa amefungwa tangu mwezi wa Septemba 2023, mwanahabari huyu alipatikana na hatia ya "kushiriki katika ufichuaji wa kimakusudi wa habari zinazohusiana na utekaji nyara, upenyezaji, shughuli za ufuatiliaji wa sauti na kuona au data iliyokusanywa".

Alikamatwa na kuzuiliwa kwa wiki moja mwezi Machi 2022, baada ya kuchapishwa kwenye tovuti ya Mosaïque FM habari zinazohusiana na kuvunjwa kwa "seli ya kigaidi" na kukamatwa kwa wanachama wake. Waandishi wa habari na wawakilishi wa mashirika ya kiraia walikusanyika mjini Tunis siku ya Jumatano kumuunga mkono Bw. Guesmi na kutaka kuachiliwa kwake "mara moja".

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya ndani na kimataifa yametoa wito kadhaa wa kuachiliwa kwake, na kushutumu kifungo chake cha miaka mitano jela kama "mbinu isiyofaa ya kutaka kunyamanzisha vyombo vya habari" na "kizuizi kikubwa kwa mfumo wa mahakama". Mashirika haya yasiyo ya kiserikali yanasikitishwa na kushuka kwa uhuru nchini Tunisia tangu Rais Kais Saied achukue mamlaka kamili mnamo Julai 25, 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.