Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Tunisia: Kiongozi wa upinzani Rached Ghannouchi aanza mgomo wa kula

Kiongozi wa kihistoria wa chama cha kihafidhina cha Ennahdha, Rached Ghannouchi, ameanza mgomo wa kula kwa siku tatu tangu Ijumaa, Septemba 29. Akiwa na umri wa miaka 82 na kufungwa tangu katikati ya mwezi Aprili, kiongozi huyo wa upinzani ananuia kushutumu kesi dhidi yake na dhidi ya "wafungwa wa kisiasa (...) waliokamatwa na kuwekwa jela na Kaïs Saïed", amesema mwanasheria wake.

Kiongozi wa chama cha Ennahdha, Rached Ghannouchi, hapa ilikuwa Tunis mnamo Julai 19, 2022.
Kiongozi wa chama cha Ennahdha, Rached Ghannouchi, hapa ilikuwa Tunis mnamo Julai 19, 2022. AP - Hassene Dridi
Matangazo ya kibiashara

Rached Ghannouchi, ingawa yuko jela, anahamasisha kupinga mashtaka anayokabiliana nayo nchini Tunisia. Mashtaka ya "kisiasa" na "yasiyo na msingi" machoni pake. Kiongozi wa Ennahdha pia anataka kuonyesha uungaji mkono wake kwa mpinzani mwingine wa kisiasa: Jawhar Ben Mbarek, mwasiasa wa mrengo wa kushoto wa chama cha National Salvation Front. Mwanasiasa huyu, mkosoaji wa Rais Kaïs Saïed, yeye mwenyewe anazuiliwa tangu mwezi wa Februari na amekuwa kwenye mgomo wa kula kwa siku tano.

Na ni kwa kuzingatia njia hii ambapo Rached Ghannouchi pia ameacha kula, tangu siku ya Ijumaa Septemba 29, kwa muda wa siku tatu. Mmoja wa wanasheria wake, Wakili Mounia Bouali, amehojiwa na Amélie Tulet: "Bwana Rached Ghannouchi anataka asikike na wasikike wafungwa wote wa kisiasa ambao kwa sasa wako katika magereza ya Tunisia baada ya kukamatwa na Kaïs Saïed, ili kutoa shinikizo kwa mamlaka kukidhi mahitaji yao na maombi yao. Rais huyu amekiuka Katiba halali na matakwa ya watu wa Tunisia waliomchagua kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 2014.

"Rached Ghannouchi na viongozi wa kisiasa wana suluhisho moja tu: kutoa sauti zao kupitia mgomo wa njaa. Madhara yake, wao huweka afya zao katika hatari kila wakati. Hasa Rached Ghannouchi, ambaye ni mzee. Ana umri wa miaka 82 na ana matatizo mengi ya kiafya,” amengeza wakili huyo.

Rached Ghannouchi alihukumiwa mwezi Mei mwaka mmoja jela kwa kutetea ugaidi. Anashutumiwa pia kwa kusema kuwa nchi kuna hatari iingie katika vita vya wenyewe kwa wenyewe ikiwa wapinzani "wataangamizwa".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.