Pata taarifa kuu

Tunisia: Mchora vibonzo anazuiliwa kwa kuchora katuni inayomkejeli waziri mkuu

Muungano wa wanahabari nchini Tunisia umelaani hatua ya mamlaka kwenye taifa hilo kwa kumzuilia mchora katuni maafuri kwenye taifa hilo.

Mchora vibonzo huyo anazuiliwa kwa kuchora katuni inayodaiwa kumkejeli waziri mkuu wa Tunisia
Mchora vibonzo huyo anazuiliwa kwa kuchora katuni inayodaiwa kumkejeli waziri mkuu wa Tunisia AP - Slim Abid
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa yao, waandishi wa habari nchini Tunisia wametoa wito wa kuachiwa haraka kwa Tawfiq Omrane.

Omrane ameshtakiwa kwa makossa ya kuchora kibonzo kinachodaiwa kumkejeli waziri mkuu wa Tunisia Ahmed Hachani.

Kwa mujibu wa wakili wake, mwanahabari huyo alichukuliwa nyumbani kwake kabla ya kupelekwa katika afisi za usalama wa kitaifa katika mji wa Mégrine, karibu na jiji kuu, Tunis, kwa maagizo kutoka kwa afisi ya mwendesha mashtaka ya umma.

Omrane anatambuliwa pia kwa uchoraji vibonzo vya kuchekesha kuhusu rais Kais Saied.

Mamlaka nchini Tunisia imekuwa inatuhumiwa kwa kuendelea kuwazuilia wakosoaji wake wa kisiasa katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.