Pata taarifa kuu

Tunisia: Maelfu ya watu wanaandamana kupinga mzozo wa kijamii na kiuchumi

Maelfu ya watu wamefanya maandamano siku ya Jumamosi kwa wito wa Chama Kikuu cha Wafanyakazi wa Tunisia mbele ya makao makuu ya serikali mjini Tunis kupinga kuzorota kwa hali ya kijamii na kiuchumi nchini Tunisia.

"Hali ya kiuchumi na kijamii inaendelea kuwa mbaya," amesema katibu mkuu wa chama kikuu cha wafanyakazi, Noureddine Taboubi, katika hotuba kwa waandamanaji, akisikitishwa "kushindwa (kwa viongozi) kuunda sera na chaguzi za kitaifa".
"Hali ya kiuchumi na kijamii inaendelea kuwa mbaya," amesema katibu mkuu wa chama kikuu cha wafanyakazi, Noureddine Taboubi, katika hotuba kwa waandamanaji, akisikitishwa "kushindwa (kwa viongozi) kuunda sera na chaguzi za kitaifa". AP - Hassene Dridi
Matangazo ya kibiashara

Hasira imetanda nchini Tunisia. Maelfu ya watu wameandamana siku ya Jumamosi Machi 2 mjini Tunis kwa wito wa Chama Kikuu cha Wafanyakazi cha Tunisia (UGTT) kupinga kuzorota kwa hali ya kijamii na kiuchumi nchini humo.

"Hali ya kiuchumi na kijamii inaendelea kuwa mbaya," amesema katibu mkuu wa chama kikuu cha wafanyakazi, Noureddine Taboubi, katika hotuba kwa waandamanaji, akisikitishwa "kushindwa (kwa viongozi) kuunda sera na chaguzi za kitaifa".

Amebaini kwamba "mazungumzo ya kijamii na kiuchumi yamezuiliwa kabisa leo", akisisitiza kwamba uwezo wa Serikali wa kulipa madeni yake ya nje mwaka 2023 " umewaumiza raia na uhaba wa bidhaa za msingi ".

Uchumi wa Tunisia umesimama na ukuaji wa 0.4% tu mnamo 2023 na kiwango cha ukosefu wa ajira ambacho kilifikia 16.4% mwishoni mwa mwaka 2023 (ikilinganishwa na 15.2% mwishoni mwa mwaka 2022), kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu.

Upungufu wa mara kwa mara wa unga, sukari au mchele

Nchi hiyo pia imetikiswa na mivutano ya kisiasa tangu mapinduzi ambayo Rais Kaïs Saïed alijipa mamlaka kamili mnamo Julai 2021.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.