Pata taarifa kuu
UHURU WA HABARI

Mwandishi wa habari anahofia maisha yake baada ya uchunguzi kuhusu jeshi la Malawi

Mwandishi wa habari wa Malawi ambaye aliikimbia nchi yake kuelekea Afrika Kusini amesema siku ya Alhamisi kwamba anahofia maisha yake kufuatia makala yake iliyoripoti ubadhirifu unaohusu kandarasi ya ugavi kwa jeshi.

Aliamua kujificha, kisha kukimbia nchi, wakati vyanzo vya karibu vya serikali vilimwambia kwamba atakamatwa kwa makala hayo.
Aliamua kujificha, kisha kukimbia nchi, wakati vyanzo vya karibu vya serikali vilimwambia kwamba atakamatwa kwa makala hayo. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Gregory Gondwe, mkurugenzi wa Jukwaa la Uandishi wa Habari za Uchunguzi, alichapisha mwezi Januari matokeo ya uchunguzi unaoshutumu jeshi hilo kuingia mkataba wa kununua magari ya kijeshi yenye thamani ya dola milioni kadhaa na kampuni inayohusishwa na mfanyabiashara Mwingereza mzaliwa wa Malawi ambaye kwa sasa yuko chini ya uchunguzi wa rushwa.

Aliamua kujificha, kisha kukimbia nchi, wakati vyanzo vya karibu vya serikali vilimwambia kwamba atakamatwa kwa makala hayo. "Nilijikuta hatarini," amesema katika mahojiano na shirika la habari la AFP. "Jeshi linashuku kuvuja ndani ya safu zao, na wanadhani kuwa kuninyamazisha kutatatua tatizo."

Baada ya maandamano ya mashirika ya kutetea haki za binadamu, yakiwemo Amnesty International na Human Rights Watch, maafisa wa serikali walimhakikishia kuwa yuko salama kurejea. Lakini Gregory Gondwe anasema hawaamini.

Wanaweza kujifanya kuwezesha kurudi kwangu, lakini kwa kweli hakuna kinachofanyika ili kuhakikisha usalama wangu,” anaeleza, akiongeza kuwa hakuna mtu ambaye amewasiliana naye moja kwa moja kutoka kwa mamlaka. 

Siku mbili baada ya kutoroka nchi, Bw Gondwe alipokea ujumbe wa kutisha kutoka kwa kamanda wa jeshi akimshauri "kubaki Afrika Kusini", kulingana na shirika la Reporters Without Borders, ambalo limesema: kutiwa wasiwasi na hali ya mwanahabari huyu.

"Hakuna mwandishi wa habari anayepaswa kuadhibiwa kwa kufichua ufisadi katika jeshi," RSF iliongeza siku ya Jumatano. Bwana Gondwe mara moja alichukulia kwa uzito taarifa kwamba mamlaka ilitaka kumkamata kwa kuhatarisha usalama wa nchi. Kwa kweli alikuwa amepitia hali kama hiyo mnamo mwaka 2022.

"Hatari ya hali yangu kubadilika na kuwa "ajali" ambayo tungepata maelezo ya kuaminika ni ya kweli," amesema. Anakusudia kurejea Malawi wakati watu waliomsaidia katika uchunguzi wake watasema kwamba anaweza kufanya hivyo bila kutishiwa.

"Kutokuwepo kwangu pengine kunaonekana kuwa jambo zuri na serikali iliyopo madarakani, kwa sababu wanajua kuwa ufichuzi wetu unaweza kupunguza nafasi yao ya kusalia madarakani baada ya uchaguzi wa mwaka ujao," ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.