Pata taarifa kuu

Malawi yaondoa vikwazo vya viza kwa nchi 79

Nairobi – Malawi imeondoa vikwazo vya viza kwa wasafiri kutoka mataifa 79 katika juhudi za kukuza utalii na biashara nchini humo.

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera.
Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera. © State House Malawi
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa usalama wa ndani, Ken Zikhałe, katika notisi kwenye gazeti la serikali siku ya Jumatano, alifanyia marekebisho kanuni za uhamiaji, na kuondoa vizuizi vya visa kwa raia kutoka Uingereza, China, Urusi, Ujerumani, Australia, Canada, Ubelgiji, Ghana, Gambia, Sierra Leone, Ufaransa na nchi nyengine.  

Raia kutoka nchi za Jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa Afrika (Sadc) na soko la pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika (Comesa) pia wameondolewa vikwazo hivyo vya viza.

Hatua hii ya serikali haijumuishi nchi zinazowataka raia wa Malawi kuwa viza wakati wakizuru mataifa hayo.

Ubalozi wa Uingereza nchini Malawi uliwataka raia wake kuchukua fursa hiyo ya serikali  kutembelea vivutio vingi vya utalii katika nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

Malawi inaungana na Kenya na Rwanda kufungua nchi zao kwa wasafiri kutoka barani Afrika bila vikwazo vya visa.

Nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zimetangaza kuingia bila visa kwa wageni kutoka bara Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.