Pata taarifa kuu

Malawi: Mfumo wa idara ya uhamiaji wakabiliwa na uhalifu wa mitandaoni

Nairobi – Mamlaka nchini Malawi imesitisha utoaji wa hati za kusafiria kufuatia shambulio la mtandaoni kwenye mfumo wa kompyuta katika idara ya uhamiaji nchini humo.

Kwa muda wa wiki mbili zilizopita, Malawi imekuwa haitoi pasi za kusafiria kwa kile maafisa walisema ni kutokana na hitilafu za kiufundi
Kwa muda wa wiki mbili zilizopita, Malawi imekuwa haitoi pasi za kusafiria kwa kile maafisa walisema ni kutokana na hitilafu za kiufundi AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Rais Lazarus Chakwera aliwaambia wabunge kwamba hatua hiyo ya kulengwa kwa idara ya serikali ni sawa na "ukiukaji mkubwa wa usalama wa taifa".

Aidha rais Chakwera alieleza kuwa wadukuzi hao walikuwa wakiomba fidia suala ambalo amesisitiza kwamba halitakubalika na kwamba serikali inajitahidi kutatua tatizo hilo.

Idadi kubwa ya watu nchini Malawi wamekuwa wakitatfuta hati za kusafiria , vijana wengi wakitafuta wakiwa na nia ya kuondoka kwenye taifa hilo kutafuta maisha bora katika nchi za kigeni.

Rais Chakwera alisema ameipa idara ya uhamiaji muda wa wiki tatu ambapo inatakiwa kutoa suluhu la muda na kuanza tena utoaji wa hati za kusafiria, huku wakisubiri kurejesha udhibiti wa mfumo huo.

Licha ya agizo hilo kwa idara ya uhamiaji, rais pia alisema suluhu la muda mrefu lenye ulinzi wa ziada litaafikiwa ilikuzia visa kama hivyo.

Kwa muda wa wiki mbili zilizopita, Malawi imekuwa haitoi pasi za kusafiria kwa kile maafisa walisema ni kutokana na hitilafu za kiufundi.

Hapo jana Jumatano mkuu wa nchi kwa mara ya kwanza aliweka wazi kuwa mfumo wa uhamiaji ulidukuliwa bila kuwataja wadukuzi waliohusika na tukio hilo.

Raia wa Malawi wamekuwa wakidai majibu kutoka kwa serikali kutoakana na suala la ucheleweshaji unaoendelea wa utoaji wa hati ya kusafiria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.