Pata taarifa kuu

Morocco: Mwanablogu aliyepatikana na hatia ya 'kumtusi' waziri ahukumiwa kifungo cha miaka miwili

Mwanablogu wa Morocco amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela kwa "kumatusi" kufuatia malalamiko kutoka kwa Waziri wa Sheria kuhusu machapisho yanayohusishwa na kesi kubwa ya ulanguzi wa dawa za kulevya, wakili wake amesema.

Mwanablogu huyo alihukumiwa na mahakama ya kwanza ya Agadir baada ya kupatikana na hatia ya "kumtusi afisa wa umma" na "kukashifu", wakili wake amesema, akielezea hukumu hiyo kuwa "kali na isiyo ya haki".
Mwanablogu huyo alihukumiwa na mahakama ya kwanza ya Agadir baada ya kupatikana na hatia ya "kumtusi afisa wa umma" na "kukashifu", wakili wake amesema, akielezea hukumu hiyo kuwa "kali na isiyo ya haki". © AFP
Matangazo ya kibiashara

Mwanablogu Mohamed Reda Taoujini ambaye aliyekamatwa wiki iliyopita katika mji wa Agadir (kusini-magharibi), alihukumiwa siku ya Jumatano jioni kifungo cha miaka miwili jela na faini sawa na euro 1,830 kufuatia malalamiko mawili ya Waziri wa Sheria, Abdellatif Ouahbi, kulingana na wakili wake Redouane Arabi.

Waziri huyo alimshutumu mwanablogu huyo kwa kumkashifu katika video mbili alizorusha mtandaoni akihoji kuwa huenda anahusishwa na biashara kubwa ya dawa za kulevya, kesi inayojulikana kwa jina la "Escobar of the Sahara", baada ya kukamatwa kwa maafisa wawili waliochaguliwa kutoka chama chake cha siasa,  cha Authenticité et Modernité (PAM), kama sehemu ya uchunguzi.

Wajumbe wa chama cha PAM ambacho kinashiriki katika serikali, Saïd Naciri, rais wa baraza la mkoa wa Casablanca (magharibi) na Abdennabi Biioui, rais wa baraza la eneo la mashariki, mashariki mwa nchi waliwekwa kizuizini mnamo Desemba 22 kwa madai ya kuhusika katika biashara hii ya haramu. Bw. Naciri pia ni rais wa klabu ya Wydad Casablanca, mojawapo ya vilabu muhimu vya kandanda barani Afrika. Hii ni mara ya kwanza kwa vigogo wawili wa kisiasa wa vyeo hivyo kudaiwa kuhusika na ulanguzi wa dawa za kulevya wa kiwango hiki nchini Morocco.

Mwanablogu huyo alihukumiwa na mahakama ya kwanza ya Agadir baada ya kupatikana na hatia ya "kumtusi afisa wa umma" na "kukashifu", wakili wake amesema, akielezea hukumu hiyo kuwa "kali na isiyo ya haki". Kulingana na tovuti ya habari ya Lakome2, Waziri wa Sheria pia aliwasilisha malalamishi dhidi ya wanahabari watatu waliozungumza kuhusu madai yake ya uhusiano na ulanguzi wa dawa za kulevya.

Uchunguzi huo unahusu jumla ya watu 25, 20 kati yao wamefungwa. Wanashukiwa hasa "kumiliki, uuzaji na uuzaji nje wa madawa za kulevya" na "ufisadi", kulingana na mwendesha mashtaka. Washukiwa hao wanaaminika kuhusishwa na Hadj Ahmed Ben Brahim, raia wa Mali ambaye anatumikia kifungo cha miaka 10 nchini Morocco kwa ulanguzi wa kimataifa wa dawa za kulevya.

Bw. Ben Brahim ambaye alipewa jina la utani la "Pablo Escobar wa Sahara", alikamatwa mnamo mwaka 2019 huko Casablanca, kama sehemu ya uchunguzi wa rekodi ya kunasa tani 40 za bangi mnamo mwaka 2015 katika malori yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.