Pata taarifa kuu

Morocco: Maelfu waandamana kutaka kusitishwa kwa uhusiano na Israeli

Nairobi – Maellfu ya raia nchini Morocco wameandamana jijini Rabat wakitoa wito kwa mamlaka kusitisha uhusiano na Israeli kutokana na mapigano ya huko Gaza.

Waandamanji wanataka uhusiano wa Morocco na Israeli kusitishwa
Waandamanji wanataka uhusiano wa Morocco na Israeli kusitishwa AP - STR
Matangazo ya kibiashara

Inaelezwa kuwa wanasiasa mbalimbali kwenye taifa hilo waliungana na raia kwenye maandamano hayo.

Morocco ilianzisha uhusiano na nchi ya Israeli mwaka wa 2020 chini ya mazungumzo yalioongozwa na Marekani.

Upinzani dhidi ya makubaliano hayo umekuwa ukionekana tangu kuanza kwa vita huko Gaza.

Tangu kuanza kwa vita katika ukanda wa Gaza, wito wa kusitishwa kwa makubaliano hayo umekuwa ukitolewa
Tangu kuanza kwa vita katika ukanda wa Gaza, wito wa kusitishwa kwa makubaliano hayo umekuwa ukitolewa AP

Haya yanajiri wakati huu wizara ya afya huko Gaza inayoendeshwa na Hamas ikisema takriban watu 28,176 wameuawa na 67,784 wamejeruhiwa katika mashambulio ya Israel kwenye eneo hilo tangu Oktoba 7, idadi kubwa ya wanawake na watoto.

Maafisa wa Israel wanasema kuwa takriban watu 1,140 waliuawa katika mashambulio yaliyoongozwa na Hamas Oktoba 7 kusini mwa Israel.

Wapiganaji wa Hamas waliwateka watu 250 wakati wa shambulio hilo na 132 bado wanazuiliwa huko Gaza, kulingana na takwimu za Israeli.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.