Pata taarifa kuu
HAKI-MGOMO

Morocco: Kiongozi wa upinzani Mohamed Ziane aanza mgomo wa kula

Kiongozi wa upinzani nchini Morocco na waziri wa zamani anayefungwa Mohamed Ziane, 81, ameanza mgomo wa kula kutaka kuachiliwa kwake, mwanawe ambaye pia ni wakili wake, ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa.

Bw. Ziane alifunguliwa mashitaka tangu Januari 10 kwa "ufujaji wa fedha za umma", katika kesi mpya ya "ubadhirifu" wa ruzuku ya umma iliyopokelewa na chama alichokiongoza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015, madai ambayo anakanusha.
Bw. Ziane alifunguliwa mashitaka tangu Januari 10 kwa "ufujaji wa fedha za umma", katika kesi mpya ya "ubadhirifu" wa ruzuku ya umma iliyopokelewa na chama alichokiongoza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015, madai ambayo anakanusha. Β© FADEL SENNA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Β 

Rais wa zamani wa chama cha wanasheria katika mji wa Rabat, Mohamed Ziane alihukumiwa mwaka 2022 kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya malalamiko kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kwa mashtaka kumi na moja, ikiwa ni pamoja na "kutusi viongozi wa umma na vyombo vya sheria", "tusi dhidi ya taasisi", " kashfa", "uzinzi" au "unyanyasaji wa kijinsia".

"Anaendelea na mgomo wake wa kula, ambao alianza siku ya Alhamisi," Ali Reda Ziane ameliambia shirika la habari la AFP, baada ya kumtembelea babake. "Nilijaribu kumshawishi aache lakini hana nia ya kutengua uamuzi wake. Hatambui anachotuhumiwa na anabaini kwamba hakuhukumiwa kwa haki," ameongeza. "Anaomba kuachiliwa kwake, kumalizika kwa kesi dhidi yake na afutiwe mashitaka."

Siku ya Alhamisi mamlaka ya gereza la Al Arjat, lililo karibu na Rabat, imesema katika taarifa kwamba mfungwa "Bwana Z." alikuwa "ametupa" trei yake ya kiamsha kinywa "nje ya seli", ikielezea tabia hii kama "kutowajibika". Hata hivyo, chanzo cha gereza kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba Bw. Ziane alisitisha mgomo wake wa kula siku ya Ijumaa asubuhi.

Kulingana na mwanawe na wakili wake, Bw. Ziane alifunguliwa mashitaka tangu Januari 10 kwa "ufujaji wa fedha za umma", katika kesi mpya ya "ubadhirifu" wa ruzuku ya umma iliyopokelewa na chama alichokiongoza wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015, madai ambayo anakanusha.

Mohamed Ziane alikuwa Waziri wa Haki za Binadamu kati ya mwaka 1995 na 1996. Mwanzilishi wa Chama cha Kiliberali cha Morocco (PML), afisa huyu mkuu wa serikali alijidhihirisha katika miaka ya hivi karibuni kupitia taarifa kali dhidi ya serikali, hasa dhidi ya idara ya ujasusi ya Morocco. Anadai kuwa alihukumiwa "kwa sababu ya maoni yake".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.