Pata taarifa kuu
RUSHWA-SHERIA

Aliyekuwa mkuu wa klabu ya Raja Casablanca azuiliwa kwa ufisadi nchini Morocco

Mkuu wa zamani wa Raja Casablanca, moja ya vilabu vikuu vya soka nchini Morocco, na naibu wake, wanazuiliwa tangu siku ya Ijumaa kwa tuhuma za kuhusika na suala la rushwa, kulingana na shirika la habari la AFP ilikinukuu chanzo cha mahakama.

Siku ya Ijumaa jaji mchunguzi katika Mahakama ya Rufaa ya Casablanca ameagiza kukamatwa kwa Aziz El Badraoui, mkuu wa Raja kati ya 2022 na 2023, mbunge Mohamed Karimine na mhandisi mstaafu, ambao walihojiwa wiki hii.
Siku ya Ijumaa jaji mchunguzi katika Mahakama ya Rufaa ya Casablanca ameagiza kukamatwa kwa Aziz El Badraoui, mkuu wa Raja kati ya 2022 na 2023, mbunge Mohamed Karimine na mhandisi mstaafu, ambao walihojiwa wiki hii. © FADEL SENNA / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Kuzuiliwa kwao kunakuja wakati maafisa wengine wa Morocco hivi karibuni wakikamatwa katika kashfa ya ufisadi na ulanguzi wa dawa za kulevya, akiwemo mkuu wa klabu nyingine kuu ya soka ya Casablanca, Wydad.

Siku ya Ijumaa jaji mchunguzi katika Mahakama ya Rufaa ya Casablanca ameagiza kukamatwa kwa Aziz El Badraoui, mkuu wa Raja kati ya mwaka wa 2022 na 2023, mbunge Mohamed Karimine na mhandisi mstaafu, ambao walihojiwa wiki hii.

Wanashukiwa kwa "ufujaji wa fedha za umma", "ubadhirifu" na "matumizi ya kughushi", chanzo cha mahakama ambacho kimeomba kutotajwa jina lake kimeliambia shirika la habari la AFP. Uchunguzi unahusu kandarasi za ukusanyaji taka zinazohusisha kampuni inayomilikiwa na Bw. El Badraoui na wilaya ya Bouznika (kusini mwa Rabat), inayoongozwa na Bw. Karimine (chama cha Istiqlal, muungano wa serikali).

Viongozi wengine wawili waliochaguliwa wamekuwa kizuizini tangu Desemba 22, wakishukiwa kuwa na jukumu muhimu katika mtandao mkubwa wa mfanyabiashara wa dawa za kulevya kutoka Mali, Ahmed Ben Brahim, aliyepewa jina la utani la "Pablo Escobar wa Sahara". Said Naciri, mwenyekiti wa Baraza la Mkoa wa Casablanca (magharibi) na mkuu wa Wydad Casablanca, na Abdennabi Biioui, rais wa Baraza la Mkoa wa Mashariki (mashariki) watasikilizwa tena wiki ijayo na jaji mchunguzi.

Uchunguzi huu unahusisha watu 25, 20 kati yao walikuwa wamefungwa. Tawi la Morocco la shirika la Transparency International lilionya mwishoni mwa Januari kuhusu ufisadi "wa kimfumo na uliokithiri" nchini humo, na kutishia "uthabiti wake wa kijamii, kiuchumi na kisiasa". Morocco iko katika nafasi ya 97 kati ya nchi 180 katika orodha ya 2023 ya ripoti ya mtazamo wa ufisadi ya Transparency International, ikipoteza nafasi tatu ikilinganishwa na mwaka uliopita na 24 katika miaka mitano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.