Pata taarifa kuu
RUSHWA-UCHUMI

Ufisadi 'unatishia utulivu' nchini Morocco, kulingana na Transparency International

Tawi la Morocco la Transparency International limebaini siku ya Jumanne kuwa rushwa "inatishia utulivu" wa nchi, ambayo imerekodi kushuka zaidi katika orodha yake ya kila mwaka katika ngazi ya kimataifa inayoorodhesha janga hili la rushwa.

Bendera ya Morocco katika jangwa.
Bendera ya Morocco katika jangwa. AFP - FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

 

Morocco imewekwa kwenye nafasi ya 97 kwenye orodha ya mwaka 2023 iliyochapishwa na Transparency International ambayo inapima mtazamo wa rushwa ndani ya sekta ya umma katika nchi 180, ikipoteza nafasi tatu ikilinganishwa na mwaka uliopita na 24 katika miaka mitano.

"Rushwa ya kimfumo na iliyoenea inatishia utulivu wa kijamii, kiuchumi na kisiasa wa nchi yetu na inahimiza uchumi wa usio halali na ulinzi wa shughuli haramu," Transparency imeonya katika taarifa. Kuchapishwa kwa safu hii kunakuja katika muktadha wa kashfa kadhaa za ufisadi ambazo zinatikisa ulimwengu wa kisiasa nchini Morocco.

Kesi inayojulikana zaidi ni ile ya Saïd Naciri, rais wa Baraza la Mkoa wa Casablanca (magharibi) na bosi wa klabu ya soka ya Wydad Casablanca, na Abdennabi Biioui, rais wa Baraza la Mkoa wa Mashariki. Viongozi hao wawili waliochaguliwa, waliowekwa kizuizini tangu Desemba 22, wanashukiwa kuwa na jukumu muhimu katika mtandao mkubwa wa mfanyabiashara wa dawa za kulevya kutoka Mali, huku Ahmed Ben Brahim, akipewa jina la utani la "Pablo Escobar wa Sahara".

Zaidi ya hayo, Transparency Maroc inabainisha katika taarifa yake kwamba wabunge 29 wamehusika katika kesi za ufisadi zilizowasilishwa mbele ya mahakama katika miaka ya hivi karibuni. Shirika hili linatoa wito kwa serikali kuchukua "kundi la kisheria la kupambana na rushwa", hasa sheria dhidi ya mzozo wa maslahi na utajiri haramu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.