Pata taarifa kuu

Mawaziri watatu wapya wateuliwa nchini Tunisia

Waziri mpya wa Uchumi na Mipango, Feryel Ouerghi, ana shahada ya udaktari na ndiye mhusika wa machapisho kuhusu migogoro ya kifedha na sera za viwango vya ubadilishaji. Anachukua nafasi ya Samir Saïed, aliyefutwa kazi mnamo mwezi wa Oktoba 2023 bila kulelezwa sababu.

Rais wa Tunisia Kais Saied akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo mwaka 2023 katika eneo la Mnihla, katika mkoa wa Ariana, nje kidogo ya Tunis, Desemba 24, 2023.
Rais wa Tunisia Kais Saied akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa mnamo mwaka 2023 katika eneo la Mnihla, katika mkoa wa Ariana, nje kidogo ya Tunis, Desemba 24, 2023. © FETHI BELAID / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Rais Kais Saied pia amemteua Fatma Thabet kama Waziri wa Viwanda, Nishati na Madini, akichukua nafasi ya Neila Gonji, aliyefutwa kazi mwanzoni mwa mwezi wa Mei 2023. Tunisia inashiriki ushirikiano na Umoja wa Ulaya unaojumuisha kipengele muhimu cha nishati.

Waziri mpya wa Ajira na Mafunzo ya Ufundi, Lotfi Dhieb, ni mkurugenzi mkuu wa zamani ndani ya wizara hii. Anachukua nafasi ya Nasreddine Nsibi, aliyefukuzwa kazi mwezi wa Februari 2023. Rais pia ameteua makatibu watatu wa serikali, wanaohusika hasa na SMEs (Biashara Ndogo na za kati) na Mpito wa Nishati.

Uchumi wa Tunisia umesimama na ukuaji wa 1.3% mwaka jana na kiwango cha ukosefu wa ajira cha karibu 16%. Nchi hiyo pia imetikiswa na mvutano wa kisiasa tangu hatua ya Rais Saied ya kujipa mamlaka kamili mnamo mwezi Julai 2021.

Katika mgogoro mkubwa wa kifedha, Tunis ilihitimisha makubaliano na shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, mnamo Oktoba 2022 kwa mkopo wa dola bilioni mbili lakini mazungumzo yalikwama pale rais alipokataa mageuzi yaliyopendekezwa na Shirika la Fedha la Kimataifa.

Tunisia inatoa hoja ya kulipa madeni yake (asilimia 80 ya Pato la Taifa) lakini inakosa ukwasi wa kuwapatia wakazi wake bidhaa za kimsingi za kutosha, jambo ambalo linasababisha uhaba wa mara kwa mara wa unga, sukari au mchele.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.