Pata taarifa kuu

Zaidi ya wahamiaji 69,000 walinaswa nchini Tunisia mwaka 2023

Tunisia imeshuhudia ongezeko kubwa la uvamizi wa wahamiaji mwaka huu, huku takriban watu 70,000 walinaswa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania kuelekea Italia. Hii ni zaidi ya mara mbili kwa kipindi kama hicho mwaka uliotangulia, kikosi cha walinzi wa taifa wamebaini siku ya Jumamosi, Desemba 9.

Kundi la wahamiaji kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwasili kwenye kisiwa cha Gran Canaria, mwezi Novemba 2005.
Kundi la wahamiaji kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiwasili kwenye kisiwa cha Gran Canaria, mwezi Novemba 2005. BOJA SUAREZ / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya wahamiaji walionaswa na mamlaka ya Tunisia imeongezeka zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita, kutoka 31,297 mwaka 2022 hadi 69,963 mwaka 2023.

Kati ya jumla hii, 77.5% walikuwa wageni, hasa raia kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara. Asilimia 22.5 iliyobaki walikuwa Watunisia.

Kuondoka na kwenda Ulaya kwa wahamiaji kumeongezeka baada ya hotuba ya Rais wa Tunisia Kais Saied, akilaani kuwasili kwa "makundi ya wahamiaji haramu" kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Maoni haya yaliibua kampeni kali dhidi ya wahamiaji, na kusababisha nchi kadhaa za Afrika kuwarejesha makwao maelfu yao.

Mnamo mwaka 2023, wahamiaji wengi waliozuiliwa (82%) walikuwa kwenye pwani karibu na Sfax, jiji ambalo liko umbali wa kilomita 150 kutoka kisiwa cha Italia cha Lampedusa.

Kuongezeka kwa kasi mpya kwa kuondoka kwa wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kulitokea msimu huu wa joto baada ya mamia yao kufukuzwa kutoka Sfax na kuendeshwa na polisi hadi maeneo ya jangwa kwenye mipaka ya Libya na Algeria.

Umoja wa Mataifa ulishutumu kufukuzwa huko, lakini mamlaka ya Tunisia ilipuuzia mbali.

Hali ya wahamiaji nchini Tunisia inatia wasiwasi. Vizuizi vimeongezeka maradufu katika kipindi cha mwaka mmoja na wahamiaji kufukuzwa kwa pamoja kwenda Libya na Algeria kunaendelea, na kuhatarisha maisha ya wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.