Pata taarifa kuu

Tunisia: Wahamiaji wa Sudan walazimika kuishi mitaani kutokana na shida wanazozipata

Idadi ya wahamiaji wa Sudan wanaokimbia Libya au nchi yao ya asili imeongezeka katika miezi ya hivi karibuni nchini Tunisia. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) lilisajili Wasudan 330 huko Sfax mwezi Julai, na kulikuwa na ongezeko la wahamiaji wapya kusini mwa Tunisia katika mwezi huo: watu 860 walijiandikisha, 67% ya watu hao, walikuwa Wasudan. Wengi wanaishi katika mazingira hatarishi.

Wahamiaji wa Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiandamana dhidi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi huko Zarzis, Tunisia, Februari 2022.
Wahamiaji wa Kusini mwa Jangwa la Sahara wakiandamana dhidi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi huko Zarzis, Tunisia, Februari 2022. AFP - FATHI NASRI
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum huko Zarzis na Médenine, Lilia Blaise

Mbele ya ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Zarzis, kusini mwa Tunisia, Wasudan zaidi ya mia moja wanasubiri kuitwa kwa nambari zao na majina yao ili kujiandikisha na shirika hilo. Abdulneijar amekuwa akija kila siku tangu alipowasili kutoka Libya wiki moja iliyopita. Alifanya safari ya siku nne jangwani: “Tayari nimejiandikisha, lakini hapa nasubiri karatasi rasmi ili nipewe miadi. "

Baada ya saa moja ya kusubiri, anapokea karatasi yenye miadi ya mahojiano yaliyopangwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Anapaswa kusubiri miezi miwili, bila kujua pa kwenda au kupata chakula. "Kwa keli hali ngumu. Tangu nilipowasili, sioni msaada wowote au usaidizi wowote kutoka kwa mashirika ya kibinadamu. Kwa bahati nzuri, hadi sasa, wenyeji wengine hunipa mkate au maji, lakini sikutarajia hilo, "anasema.

Katika barabara ya kuelekea Medenine, kilomita chache tu, Wasudan wengi wanaishi katika vituo vinavyosimamiwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, ambalo haliruhusu upatikanaji wa waandishi wa habari, au hata mitaani, kama Ousmane Ali, ambaye aliwasili Tunisia tangu mwaka 2018. Mnamo 2019, kadi yake ya usajili ya UNHCR iliisha, na hakuweza kuirejesha. Lakini anataka kubaki nchini Tunisia: "Nimekuwa na matatizo mengi, lakini sijisikii kunyanyaswa au kudhalilishwa hapa. Tatizo ni kwamba kuna kazi ndogo ndogo kwa ajili yetu. Lakini nina marafiki wa Tunisia ambao walinisaidia. "

Katika miji ya Médenine na Zarzis, kusini mwa Tunisia, wengi wanaishi mitaani, wakisubiri kupata msaada.

Wengi wa wahamiaji hao wanasema hawaogopi ghasia na ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi ambao ambazo zilishuhudiwa nchini humo katika miezi ya hivi karibuni. Kwao, Tunisia inasalia kuwa nchi mbadala pekee ikilinganishwa na hali inayojiri katika nchi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.